advert

http://

Tuesday 29 October 2013

RAY C AWA BONDIA,AMTWANGA HUYU DADA WA BONGO MOVIE.


Na Musa Mateja
KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.



Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.


Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.

Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.

Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.

Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.

Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo gazeti hili lilimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.

“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.

“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha. 

Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.


Source:GPL



Msanii wa Hip pop Ney wa mitego 'TRUE BOY' Amewaonyesha uso wa mbuzi Basata ambao awali walimwonya kutokana na tabia yake ya kuvaa mlegezo "KATA K" akiwa jukwaani kwa madai ya kuidhalilisha sanaa hiyo..


Katika hali ya kushangaza kabisa Msanii huyo ameonekana kupuuzia agizo hilo la basata na kendelea kuvaa mlegezo wakati akilishambulia Jukwaa huku akishangiliwa na mashabiki lukuki wa Bongo Fleva .


Tukio hilo lilitokea jana wakati wa Show ya FIESTA DAY 2 iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaderz Club alipokuwa akiwapagawisha wapenzi wake na kibao chake cha "MUZIKI GANI" Akiwa sambamba na Msanii mwenzake Diamond Platinumz.

Sasa wapenzi wa Bongo fleva wanasubiri Rungu la Basata liweze kufanya kazi yake huku wengi wakionekana kumtetea kwa kudai kuwa kila mtu ana aina ya maisha yake 'Life Style'

Leo hii rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria msiba wa Balozi Abrahamu Sepetu (Baba mzazi wa Wema Sepetu) uliotokea hapo juzi jijini Dar es Salaam.


Mheshimiwa kiwete amefika msibani akiongozana na mkewe hapo kutoa pole kwa familia hiyo kwa  kuondokewa na Balozi Sepetu ambaye hapo alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali nchini ikiwemo ya kuwa waziri wa mambo ya nje kwenye miaka ya sabini (70) kabla  ya kuwa balozi wa urusi kwenye kipindi cha miaka ya 80. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Mchumba huyo wa mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Diva alitoa kali ya mwaka baada ya kuzimia ghafla huku akitokwa na mapovu kinywani baada ya kunaswa na OFM akijiuza. 


Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita maeneo ya Kimboka, Buguruni, Dar ambapo msichana huyo pamoja na ‘madadapoa’ wenzake walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu bila kificho.

Mara baada ya kuona wenzake wakiwa mikononi mwa nguvu za dola katika kamatakamata ya polisi, mrembo huyo ambaye baadaye alijitambulisha kama mchumba wa mtu, alianguka ghafla na kuzimia kiasi cha kuzua hofu miongoni mwa machangu wenzake walioangua kilio wakidhani mwenzao amekata ringi (kufa).

Baada ya muda msichana huyo alirejewa na fahamu akiwa mikononi mwa polisi na kuanza kuangua kilio akiomba asikamatwe kwa kuwa yeye ni mchumba wa mtu na atakuwa kwenye wakati mgumu kama mchumba’ke atajua anajiuza.

“Naomba msinikamate. Mimi ni mchumba wa mtu afande. Mtaniweka kwenye wakati mgumu kama akijua nilikuwa nikijiuza. Jamani nitamkosa mchumba wangu Luka,” alisema mrembo huyo huku akiomba maji ya kunywa.

Hata hivyo, kilio chake hakikuwazuia ‘OFM’ kufanya kazi yake ndani ya Kituo cha Polis.


GPL

Katika mahojiano yake na gazeti moja hapa jijini nimesikia aunt lulu akisema wanaume wamemla sana uroda bure kwa miaka mingi sana bila faida, 


ila kwa sasa harudii kosa hilo ni mwendo wa faranga kwa kwenda mbele, sincerely kwa hizo pics hapo juu nani anaweza akawa na mwanamke kama huyu and shower her dollazzzz?? men also haaaaa as they say one man's meat is another man's poison.

 kwahio tusiliongelee sana ila wakati mwingine maneno tunayaongea ktk media yanafanya wasanii waonekane kituko katika jamii kabisa na akili zako na unajitambua wewe ni msanii  unaweza ukaongea pumbaless kama hii na watu wakasoma na kukuelewa ??

WANAUME WAMENILA URODA BURE MIAKA MINGI SANA BILA FAIDA SASA HIVI SIRUDII KOSA NG'OO: ANT LULU!

hiki ni nini wajameni? nikisema mtasema Sintah anaongea?? niko hapa kwaajili ya kurekebisha watu na jamii inachukulia wasanii kama kioo chao, sasa kwa matendo haya ya lulu na alivyoongea wengine tunaonekana vipi,

ni wakati umefika sasa tujue kuna wasanii na wanaotafuta umaarufu ili ya kwao yawaendee eg kupata mabwana na wanawake 

yaani nimekereka sana na hii kauli ya Aunt Lulu so sasa hivi anauza rasmi na ameamua kujitangaza kama tunavyojua biashara ni matangazo ?? God  forbid.


i do the seeking n u do the judging...

Gari la Madam Rita, Mercedes Benz lateketea kwa moto likiwa barabaraniGari aina ya Mercedes Benz la Rita Paulsen aka Madam Rita limeteketea kwa moto likiwa barabarani Jumamosi iliyopita, Oct 26.
Hata hivyo kwenye gari hilo lililozimika barabarani na kuanza kuwaka moto, hakuwemo Madam Rita bali dereva wake, Julius Kanwakaita.
Chanzo kilichopelekea gari hilo kuwaka moto hakijafahamika mara moja.
August 21 mwaka jana, ofisi za kampuni yake ya Benchmark Productions zilizopo Mbezi Beach ziliteketea pia kwa moto

Daktari wa Michael Jackson Aliyekuwa daktari wa mfalme wa Pop duniani marehemu Michael Jackson, Conrad Murray ameachiwa huru baada ya kukaa jela miaka miwili kwa kosa la kusababisha kifo cha Michael bila kukusudia.
Dr. Murray ambae mwaka 2011 alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela, kifungo  ambacho mama yake Michael Jackson alisikika akisema kwa uchungu mahakamani hapo “haitoshi”, ameachiwa huru mapema kutokana na mwenendo wake katika kutumikia kifungo hicho.
Kuachiwa kwa Murray mwenye miaka 60, huenda kukaikasirisha zaidi familia ya Michael Jackson na mashabiki wake ambao wanaamini kifo chake kilisababishwa na daktari huyo.
Kwa mujibu wa Sky News, bado mahakama imezuia kutumika kwa leseni yake ya udaktari katika majimbo matatu ambayo alikuwa akifanyia kazi hapo awali.
Lakini ripoti kutoka kwa watu wa karibu wa Murray zinadai kuwa huenda akafuatilia kwa undani uamuzi huo na kufanya jitihada za kuzirejesha utumikaji wa leseni yake katika majimbo hayo.
Conrad Murray alifungwa jela baada ya kukutwa na hatia ya kusababisha kifo cha Michael Jackson mwaka 2009, kwa kumpa dawa zilizomzidi nguvu (Overdose) na kupelekea kifo chake.

source:Times fm.


Linex azipa likizo ya miezi minne kumbi za Dar, asema hatofanya show kwenye kumbi za Dar hadi February mwakaniMkali wa mashairi yenye ujumbe mzito Linex Sunday, ameamua kuzipa likizo kumbi za bongo kwa muda wa miezi minne kuanzia leo (October 28,2013) hadi February 14,2014. Ambayo itakuwa siku yake ya kuzaliwa.
Mwanahisa huyo wa kampuni ya Kigoma All Stars ameweka katika maandishi uamuzi wake kupitia Instagram jana, muda mfupi kabla hajapiga show ya mwisho kwa mwaka huu aliyoifanya jana usiku Club Billicanas.
“[ @ ] linexsundaymjeda Najiandaa kwenda bills kwenye show ya Bob jr show ambayo itakua ya mwisho kufanya kwenye club za dar mpaka next year 14/2/2014 siku ambayo itakua ni b day yangu na siku hiyo ntaitumia kuintroduce Muziki wangu mpya ambao kila mtu atanishangaaa so kama uko dar lets meet there#Voa”. Ameandika Linex.
Uamuzi wake unaweza kukupa maswali mengi, kwa nini hivi, lakiini katika post yake ya pili, Sunday Mjeda alisisitiza na kutoa sababu kwa ufupi, “Yah sure Najipanga#Voa”


Chris Brown anaweza kufungwa jela miaka minne baada ya kumpiga mtu ngumi na kumchana puaMwimbaji wa ‘Fine China’ Chris Brown, ametupwa selo za polisi huko Washington, D.C, baada ya kumpiga mtu mmoja asiyemfahamu na kumjeruhi usoni.
Kwa mujibu wa TMZ Chris  na mlinzi wake walikamatwa jumapili asubuhi, na kwamba Chris alimpiga ngumi usoni mtu huyo majira ya saa kumi na nusu alfajiri nje ya hotel baada ya kutokea hali ya kutoelewana kati yao.
Mtu huyo aliyepigwa na Chris aliiambia TMZ kuwa ngumi ya Chris imepasua pua yake na inambidi leo (jumatatu) aende hospitali kufanyiwa upasuaji.
 Amesema yeye sio shabiki wa Chris na alikuwa anawapiga picha wasichana wawili ambao walikuwa wanapiga picha mwimbaji huyo nje ya hotel, na haelewi ni kwa nini Chris alikuwa kichaa vile na kumshambulia.
Hata hivyo mtu huyo amesema angeweza kumsamehe Breezy kama angeomba msamaha pale pale, lakini sasa hivi atamfunguliaa kesi dhidi yake na tayari ameshampata mwanasheria.
Lakini chanzo ambacho kiko karibu na Chris Brown kimesema kuwa mtu huyo hakuwa anataka kupiga picha nje ya hotel, bali alikuwa anataka kuingia kwenye ‘tour bus’ ya Chris ili apige picha akiwa ndani, na mwimbaji huyo alikuwa anajaribu kumzuia.
Kwa mujibu wa sheria za Washington, D.C, endapo Chris atapatikana na hatia anaweza kufungwa jela miaka minne.
Tukio hili linamuweka matatani zaidi mwimbaji huyo ambae bado yuko katika probation ya adhabu aliyopewa baada ya kumpiga mpenzi wa zamani ‘Rihanna’mwaka 2009.
Hii inaweza kutumiwa na mahakama kuwa Breezy amekiuka masharti ya probation hiyo.

Muhudumu wa kiume wa baa moja maarufu iliyopo Posta Jijini Dar hivi karibuni alinaswa akifanya ufuska kwa kumnyonya maziwa hadharani mteja wake wa kike.
 
Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa pia na wahudumu wa baa hiyo  lilitendwa  na  jamaa  huyu  kwa  mrembo  ambaye  alionekana  kunywa  pombe  kupita kiasi , hali  iliyomfanya  asijitambue
 
 1
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Chambuso alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya menejaa wake kufika na kushuhudia tukio hilo, hali  iliyomlazimu  meneja  huyo  kuchukua   uamuzi  mgumu  wa  kumtimua  kazini.

Rapper Young Killer anampango wa kuingiza hizi T Shirt sokoni hivi karibuni ila anachosubiri ni Mtazamo wa mashabiki zake kuhusu T Shirt Hizi.

Diamond kuja na video ya Diamond Platinumz anaendelea kuuongezea maisha marefu wimbo wa ‘Number One’, baada ya kuifanya Remix ya wimbo huo na msanii toka Nigeria ‘Davido’ ikiwa na muunganiko wa style ya ‘Ngololo’ na ‘Skelewu’, sasa ameamua kuwa serious zaidi na kufanya video ya ngoma hiyo (remix).
Diamond amefunguka kuhusu kuwepo kwa video hiyo kupitia Instagram, ambapo ameonesha pia nia ya kuwaalika watu ambao wanapenda kuwa sehemu ya video hiyo, ‘Do you wanna be a part ov it..? Aliuliza Diamond.
Kwa maelezo ya Diamond aliyoyaweka jumamosi kwenye Instagram, video hiyo ilitakiwa kufanyika jana jumapili, lakini hakuna taarifa za kufanyika video hiyo hapo jana, huenda video hiyo ikafanyika leo.
C.E.O wa Wasafi, aliweka picha inayoonesha yuko studio na 'Skelewu hit maker' Davido wakiipika remix ya Number One.
"[ @ ] diamondplatnumz I said NGOLOLO Dance, and he said Nah man! SKELEWU Dance... then we decided to put it in a song....and show each other what we gat, we are on tommorow for the new Video #NumberOneRemix @Diamondplatnumz ft @lifeofdavido .. Do you wanna be a part ov it...?" Aliandika Diamond.

Baada ya uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water front kumpata Rais mpya wa TFF kati ya Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi, hatimaye TFF imepata Rais mpya ambaye ni Jamal Malinzi.
Mashuhuda waliokuwepo hapo ukumbini wanasema kwamba mpinzani wa Jamal Malinzi alitoka kabla ya utaratibu mzima wa uchaguzi kuisha. Baada ya matokeo kutangwaza Jamal Malinzi alimzidi kura Athumani Nyamlani na hatimaye kupata nafasi ya kumrithi Leodigar  Tenda.

Kama ulikuwa hujui ni kwamba  Rais huyu wa TFF Jamal Malinzi ndiyo baba wa Diva Loveness wa Ala za Roho ya Clouds FM

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania kwa vijana chini ya miaka 20 imeanza vizuri kampeni zake za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa vijana chini ya miaka 20 baada ya kuichapa Msumbiji 10-0 katika mechi iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Vijana hao wa Tanzania waliianza mechi hiyo kwa kasi, ambapo katika dakika ya 6 walipata bao la kwanza lililofungwa na Neema Paul baada ya kupata pasi ya Therese Yona.

Mfungaji wa bora wa mashindano ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika

Nigeria mwaka huu, Shelder Boniface aliiandikia Tanzania bao la pili katika dakika ya 24.

Kama hiyo haitoshi, vijana wa Tanzania walizidi kulisakama lango la Msumbiji, ambapo katika dakika ya 32 Tanzania ilipata bao la tatu ambalo lilifungwa na Deonisia Daniel kwa mpira wa faulo uliokwenda moja kwa moja nyavuni.

Katika dakika ya 41 vijana wa Tanzania ambao waliibuka mabingwa kwa upande wa wanawake katika mashindano ya Airtel Rising Stars yaliyofanyika Nigeria walipata bao la nne ambalo lilifungwa na Amina Ali kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

Vijana hao wa Tanzania walifunga bao katika dakika ya 45, lakini likakataliwa na hivyo kwenda mapumziko ikiongoza 4-0.

Kipindi cha pili Tanzania ilianza kwa kasi tena na kupata bao la tano katika dakika ya 47 ambalo lilifungwa na Neema Paul baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Therese Yona.

Tanzania ilipata bao la sita ambalo lilifungwa na Shelder Boniface baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Msumbiji kutokana na shuti la Stumai Abdallah.

Dakika ya 82, Tanzania iliandika bao la saba lililofungwa na Amina Ali kwa shuti kali, pia dakika 86 Tanzania iliandika bao la nane kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Deonisia Daniel baada ya Shelder kuangushwa katika eneo la hatari.


Vijana hao wa Tanzania hawakutosheka na ushindi kwani katika dakika ya 89 walipata bao la tisa lililofungwa na Amina Ali, pia katika dakika ya 90 walifunga bao la 10 lililofungwa na Stumai Abdallah.


Kwa taarifa tulizozipata hivi sasa ni kwamba Jamal Malinzi ameshinda kitu cha urais wa shirikishi la soka nchini TFF baada ta kumshinda mpinzani wake Athumani Nyamlani.


Pia Wallace Karia amewabwaga Iman Madega na Ramadhan Nassib katika kiti cha umakamu, kwa taarifa zaidi endelea kutembelea mtandao huu

Sunday 27 October 2013

Ney wa Mitego apewa Salaam zake na Baraza la Sanaa Tanzania,apigwa marufuku kuvaa mlegezo.


Ney wa Mitego 1Ney wa Mitego ambae ni staa wa single za ‘muziki gani’ na ‘salamu zao’ amethibitisha kupewa barua na baraza la sanaa Tanzania ikiwa ni onyo la kutoendelea kuvaa suruali mlegezo kwenye majukwaa mbalimbali anayoonekana.

Kwenye interview yake na millardayo.com Ney amesema alipigiwa simu sana na namba moja lakini alikua amelala, alipoamka akakuta missedcalls nyingi so ikabidi apige ndio akaambiwa BASATA kuna barua yake ambapo baada ya kushindwa kwenda alipelekewa Manzese.
Ney anasema ‘sielewe kama BASATA ndio wameamua kudili na milegezo, sijaelewa wao wanaangalia nini zaidi, nimejaribu kuuliza wakasema nikiendelea watanifungia kazi zangu, ni kweli navaa mlegezo lakini kuna vitu vingi sana vya kufanyia kazi wao kama BASATA manake tunaibiwa kazi zetu kila siku mbona hawashughulikii hizo?’ mi tangu niko shule mlegezo ni tatizo langu kubwa ila nitajitahidi kupunguza japo nashangaa nimeandikiwa barua mimi mwenyewe wakati kuna wasanii wanavaa mlegezo hata kuliko mimi’
Ney wa Mitego
Source:Millardayo.



Ukraine ProtestLeo October 26 2013 ndio Wanawake nchini Saudi Arabia wamepanga kuandamana kupinga wao kunyimwa kuendesha magari sehemu yoyote nchini humo ikiwa ni nchi pekee duniani ambayo inakataza Wanawake kuendesha magari hata kama wanaweza.

Unaambiwa kwa sasa Mamlaka za Saudi Arabia zimewaonya Wanawake hao kutoandamana  katika maandamano hayo yatakayokua ya aina yake na ya tatu kutokea nchini humo toka mwaka 1990 ambapo Wanawake kadhaa walikamatwa na wengine kuachishwa kazi, onyo hilo linakwenda pia kwa Mwanamke yeyote ambae amepanga kuendesha gari.
Msemaji wa Serikali amesema Mwanamke yoyote atakae endesha gari leo atachukuliwa hatua za kisheria ambapo wakati siku hii ya kuandamana ikisubiriwa Wanawake kadhaa wa Saud Arabia tayari walishaweka video zao wakiendesha magari sehemu mbalimbali za Saudia lakini mpaka sasa hawajakamatwa.
Mpaka sasa zaidi ya watu elfu 17 wamesain kura ya ndio itakayo waruhusu Wanawake wa Saudi kuendesha magari ambapo pia idadi ya Wanaume wanaosupport imeendelea kuongezeka kwa kasi.
saud arabia 7
saud arabia 8
saudia 4



 Picha Zaidi Ziko Hapa



Kwenye toleo jipya la 25 la jarida la GQ Rihanna anaonekana kwenye cover la jarida hilo kwa style hii. Jarida hili linatoka October 31 2013. Picha zingine ziko hapa.



Dunia ilishtuka miaka 3 iliyopita baada ya rapper Bow Wow kutangaza kuwa amepata mtoto wa Kike. Bow Wow amekuwa akiweka picha za mtoto wake na za Mama yake Miss Joie kwenye account yake ya Instagram kitu kinacho onyesha mahusiano mazuri kati yao.


 Noorah alia na muziki wa bongo, awapinga wanaosema wana pesa nyingi bank, "muziki umekuwa na siasa nyingi"Noorah aka Baba Styles, ambae ni moja kati ya wasanii waliofanya vizuri sana miaka mingi katika kiwanda cha muziki Tanzania, ameutupia lawama mfumo wa game la muziki wa bongo kibiashara.
Mwana Chember ameyatoa ya moyoni wakati akipiga story na Moko Biashara aka One B, katika kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times fm.
Noorah amepiga mahesabu ya gharama na kipato kinachopatikana katika biashara hii ya muziki na kuonesha kwamba uwezekano wa kupata hasara ni mkubwa kuliko uwezekano wa kupata faida.
“Kwanza Industry ya muziki sasa hivi imekuwa kubwa sana, kwa kiasi ambacho kama mtu unataka kufanya muziki sasa hivi…kwa watu tunaofahamika kama sisi, doing music sasa hivi is doing business sio show tu. Lazima uwe unafanya biashara na ili kufanya biashara ni lazima uwe na mtaji mzuri,  kwa sababu kama mtu anapotoa single anakuwa na budget ya kufanya promotion.
“So  vitu kama hivyo vinahitaji budget kubwa sana kwa sababu right now in order to have a good video lazima uwe na sio chini ya 2 to 3 million, na hiyo ni ya director bado hujaingia kwenye maswala ya vifaa, location na kuwahudumia watu wanaoshoot..in short we need money.” Amesema Noorah.
Noorah alihit the point kwa mfano wake mwenyewe, “In short muziki sasa hivi una hitaji pesa, na nikijitazama sasa hivi mimi nimeshatumia zadi ya miaka 11 kwenye entertainment industry, the very same industry, na nikijiangalia kwenye upande wa kipato, yaani hairidhishi.”
Kuhusu watu wanaosema na kuonesha kuwa wana pesa na game linalipa, Noorah akatoa mtazamo wake.  
“Muziki wa sasa hivi umekuwa ni muziki ambao una siasa nyingi, siasa ni kile kitu ambacho unasema hata kama hakiko halisi, lakini unakisema kwa benefit flani ya baadae, kwa hiyo kuna watu ambao right now, we know wanasema kwamba they have a lot of money, lakini lengo la kusema mtu ana pesa ni kwamba kama kwa mfano wewe ni promoter uko kule Geita unamtaka yule msanii kuja kufanya show, na yeye ameshasema kwenye akaunti yake ana sio chini ya million 500 lazima ujiulize kwamba huyu mtu wewe utampa shilling ngapi? Hiyo ni mikakati tu ya kibishara tu. “
Noorah anaamini kama watu wangekuwa na access ya kucheck bank akaunti za wasanii wanaodai kuwa wana pesa nyingi bank, huenda wasikutwa hata na Million 150.
Source:Times fm.
Forbes wamtaja Michael Jackson kuwa namba moja kati ya Celebs waliofariki waliongiza pesa nyingi mwaka 2013, awafunika walio haiMfalme wa Pop, Marehemu Michael Jackson ametajwa na Forbes kuwa ni mmoja kati ya watu maarufu waliokwisha fariki ambao kazi zao zimeingiza pesa nyingi zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia October 2012 hadi October 2013.
kwa mujibu wa Forbes,Michael Jackson aliyefariki mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 50, ameingiza $160 million, kiasi ambacho ni kikubwa na kimezidi hata kiasi walichoingiza wasanii ambao bado wako hai, ambapo Madonna ndiye mtu maarufu aliyetajwa kuingiza pesa nyingi zaidi kwenye ‘100 Celebrities list’ akiwa ameingiza kiasi cha $125 million.
Hii ndiyo orodha ya ‘Top Earnign Dead Celebrity’ iliyotolewa na Forbes:
  1. Michael Jackson – $160 million
  2. Elvis Presley - $55 million
  3. Charles Schulz -$ 37 million
  4. Elizabeth Taylor - $25 million
  5. Bob Marley - $18 million
  6. Marilyn Monroe -$15 million
  7. John Lennon - $12 million
  8. Bettie Page& mwanasayansi Albert Einstein - $10million (wamefungana)
  9. Steve McQueen& mwandishi wa vitabu Theodor Geisel – 9 million (wamefungana)
  10. 10. Bluce Lee, na Jenni Revera (wamefungana)- $7 milllion

Jose Chameleone ameibuka mshindi kwenye tuzo za BEFFTA, tuzo kubwa za Ulaya kwaajili ya watu weusi ambazo huwatuza watu kwenye burudani, fashion, televisheni na sanaa.

Chameleone alikuwa ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act na alikuwa akishindana na wasanii wengine wakiwemo Rihanna na D'Banj.
Tuzo hizo zimetolewa jana Ijumaa na leo Jumamosi pia huko jijini London.
Kupitia Facebook, Chameleone ameandika kuelezea furaha yake baada ya kutwaa tuzo hiyo:
"It's hard to fully express my gratitude towards all of you who appreciate My MUSIC, and love AFRICAN music at large. You are the reason I have managed to add another onto my list and rankings. Am fresh and still jubilating with you This joyous feeling in me i congratulate my fans worldwide, we did this together i have just won BEFFTA AWARDS BEST INTERNATIONAL ACT- DR JOSE CHAMELEONE."

 Makala: Wasanii kuimba juu ya nyimbo zao wakiwa jukwaani Kujifunza au kufanya kazi bora hakuhitaji kutafuta uafadhali, bali kutafuta uhalali wa cheo na dhamana uliyopewa, hicho ndicho nachoamini mimi.
Imani hii ambayo haina dini iliyosajiliwa inanifanya nikubaliane na mtazamo wangu wa kupinga wasanii wa muziki wanaoimba kwa kufuatisha nyimbo zao jukwaani kuanzia mwanzo hadi mwisho, yaani Play back’, wakati mimi shabiki nimelipia kuona anachofanya jukwaani kiuhalisia, sio video shooting.
Cha ajabu kabla ya show utasikia ‘leo ntafanya kweli pale msikose’, ila nikifika nakuta naimbishwa na wimbo ule ule kama msanii anafanya video shooting, kufuatisha tu kile kilichoimbwa huku anafanya mbwembwe.
Huenda tunatofautiana nia na madhumuni ya kuhudhuria show ya msanii flani, mimi kwangu nia hua sio kumuona msanii, bali kumuona anatumbuiza kweli ule wimbo wake ninaokubali hadi nimeuweka kama mlio wa kuniamsha kwenda kazini, na mlio wa kupokelea simu.
 Njia sahihi ya yeye kuperfom mimi simchagulii, lakini ni mwepesi wa kuona makosa ya wazi anayofanya ambayo kwa upande wangu naona hajanitendea haki. Pamoja na kukubaliana na yote na mbwembwe zinazofanyika jukwaani, sauti ya msanii husika kuimba kweli my favourite song pale jukwaani huwa ni kitu nachokipa priority.
Kama shabiki wa show, nimekuwa nikichukizwa na kitendo cha wasanii kuimba juu ya wimbo ‘play back’,mimi binafsi kwa kuwa naamini na naona kuna wengine tena wa level hiyo hiyo wanaimba Live, sio lazima iwe na band lakini angalau wameweka CD yenye beat kavu, ama beat chorus, au beat chorus na back vocal za studio. Hapo nafurahi, kuona energy ya msanii na kupata ladha mpya pale jukwaani.
Mi ni mmoja kati ya watu walioshuhudia performance ya rapper wa Tanzania ‘Webiro Wasira aka Wakazi kwenye Jukwaa la BBA 2013 kwenye Eviction, mwezi July na kuikubali sana show yake, aliimba kweli kama nilivyomuona pia Young Killer, Stamina, Weusi, Nikki Mbishi na wengine wakifanya hivyo.
Bahati nzuri nikakutana na Wakazi na hii ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana nae, sasa baada ya salaam ilibidi nimuombe muda tupige story kidogo kwa kuwa nilikuwa na kiu ya kutaka kujua na yeye kama msanii anachukuliaje swala la kupiga ‘Play Back’.
“Kusema ukweli navyoona unapokuwa unafanya kazi kama msanii lazima uoneshe reality na maturity kwamba umekuwa kisanii.” Wakazi alinambia.
 Nilipigia mstari neno ‘reality’ kwa Kiswahili ‘Uhalisia’, na ndicho hicho nachokitaka kwenye show nazolipia mimi. Back vocal zinakuwepo kusapoti, lakini main ni kwake kweli.
 Sasa hivi mimi naona baadhi ya wasanii wa Bongo wamejikita zaidi kutafuta dancers na kulipamba jukwaa na hao dancers, ni kweli wanafanya vizuri, lakini bado sioni kama ni sababu ya wao kuacha kuimba live kwa kuwa wana dancers na wanacheza pia, eti wanachoka sana! Kwangu mimi hainishawishi, mbona wapo wanaocheza na wanaimba pia, au wale wa bendi za dansi wao wanawezaje.
Ama kwa jinsi Young Killer anaweza kuweka pia break dancers na wao wakacheza wakati anaendelea kuimba hivyo hivyo, kama wakazi aliponda na wasichana waliopamba show wakati akikamua kweli.
Nilimuuliza pia Wakazi kuhusu hili, ili nipate wazo la msanii pia kwa sababu mimi ni kama mlalamikaji tu mwenye mantiki lakini.
“Maturity ni pale ambapo unakuwa unafanya mazoezi vizuri na umejidhatiti ili uwe na uwezo wa kucheza na kuimba, na uwe unajua wapi unapumzika na sehemu gani, kwa hiyo unaweza kucheza na ukaimba vilevile.” Wakazi alinipa hii.
Hapo nikapata wazo jingine, baadhi ya wasaniii wengi wa Tanzania tena wakubwa hunishangaza sometimes, pamoja na kutaja kiasi kikubwa cha pesa wanacholipwa kwenye shows, bado utaona wakialikwa sehemu kwenye show watakuja na crew ya watu sita au saba hivi, na kati ya hao utakuta wacheza show 4, na mpiga picha na mpambe wa ziada, hakuna Dj, mtu wa back vocal, mabaunsa wenye miwani mwieusi..! wala hawana muda wa kuajiri mweledi wa mambo ya kuhakikisha sauti zinatoka vizuri ( sound engineer). Hapo ni kama wanaandaa mazingira ya kushindwa kukwepa hiyo ‘Play Back’.
Hapo utasikia wanatoa vijisababu, utasikia amecheza sana hawezi kuimba Live, au vyombo havisikiki vizuri, mic sometimes zinakata sauti.
Hapo naona umuhimu wa kumtaja Profesa Jay na kumpa big up kwa kumtambulisha Dj Choka aliyekuwa Dj wa Choka Mbaya Crew, na pia mtu wake wa back vocal aliyekariri nyimbo nyingi za Profesa, na Dj Choka ameendelea kufanya kazi na wasanii wengine kama AY,Roma, Lady Jay Dee na wengine ambao kwa pamoja wamehakuwa wakihakikisha show zinaenda vizuri kama ‘Live show kweli’.
Nilipata pia mawazo ya Banana Zorro ambae ana uwezo mkubwa wa kuimba Live tena na Band, huku akipiga gitaa. Yeye aliongea kupitia The Chart ya 100.5 Times fm. Lakini yeye alinipa point nyingine tofauti kidogo na mtazamo wangu.
““Unajua kwa kawaida sio kwamba play back ni kitu kibaya, ama play back sio kwamba sio sanaa ama msanii akifanya play back hapaform, bali aina ya jinsi anavyofanya play back. Kwa sababu hata wasanii wakubwa wanafanya play back.”
Napata kigugumizi kidogo kuiga kila wanachofanya wasanii wakubwa wa nje kuwa kitakuwa sahihi, ndo nakumbuka mwalimu wangu wa chuo Mr. Sijjo alikuwa anasisitiza kuwa ‘dhambi ni dhambi’ tu hata kama akiifanya malaika itabaki kuwa dhambi.
Lakini point yake ya mfano wa baadhi ya wasanii wa bongo wanavyofanya inanishawishi kwa kuwa imekuwa funny lakini ina maana sana ya kile nilichokuwa nikikisema mimi.
“Sasa hivi unaangalia kuna show za Akon anafanya mchanganyiko play back, lakini aina gani, make sasa hivi kinachotokewa ni kwamba mtu leo akishasikia play back ndo dah..anaondoka na CD yake tena ile yenye cover ambayo inauzwa sokoni, anaenda kuiplay back sasa kwelikweli.”
Lakini kauli hii ya Banana Zorro kuwa hata wasanii wan je pia wanafanya play back, niliirudisha tena kwa wakazi kama swali, kutaka kufahamu yeye anadhani kwa nini hata hao wanaoitwa wakubwa wanaimba sometimes juu ya wimbo, na sometimes wanasimama kweli.
“Unajuwa kwa upande wa wasanii wakubwa unakuta anaamua kufanya hivyo kwa kuwa anakuwa na show 30 katika siku 20, kwa hiyo show nyingine anaweza asiipe umuhimu sana, kuona kama kuna umuhimu wa yeye kujionesha kuwa yuko katika kiwango flani, kwa hiyo akaamua tu kuwapa show ya kawaida, kwa kuwa anajuwa tu atashangiliwa, ni kitu kibaya kusema ukweli.”
Kumbe tatizo hapa inaweza kuwa ni uchaguzi wa umuhimu wa show, kwa ufupi inamaanisha kudharau baadhi ya show. Mi naona kama msanii amedharau pesa, ni vyema angedharau kile kiasi cha pes alicholipwa ili asije kwenye show mapema. Sio, kwenda kwenye show kutimiza tu ratiba.
Kama ulipata nafasi ya kuangalia ‘Coke Studio’, utaona jinsi ambavyo wasanii wa Afrika wana uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi kwa kuimba Live kama wale wa nchi za nje, ulimuona Diamond akiiua vilivyo ‘Temptetion ya P-Square’ , na Lady Jay Dee ambae ni kawaida yake kufanya na Live.
Hii inanisababisha nikubali kabisa kuwa wasanii wa kibongo wanaweza kufanya poa sana na kuachana na ‘Play back’.
Utajiuliza inakuwaje msanii anashindwa kuimba wimbo wake Live jukwani bila hiyo CD iliyoko radioni, wakati hata katika mashindano ya kuimba kama TPF6 na EBSS, washiriki wanaimba vizuri nyimbo za wasanii hawahawa wa bongo na wa nje, wanaziimba vizuri bila Play Back. Sasa inakuwaje mwenye wimbo mwenyewe ashindwe kuutendea haki jukwaani?
Hali hii inanifanya niungane na kauli ya Master J, jaji wa EBSS wakati akitoa maoni yake kwa baadhi ya washiriki wa EBSS.
“Narudia na ntaendelea kurudia sana hili, kuna watu wanaperform chini ya hapo huko nje, na wanamiliki magari na majumba.”
Sasa kwa mtindo huu nadhani huu ndio nauita ‘unyonyaji’ kwa kuwa msanii hufanya kazi chini ya kiwango japo anafanya vizuri kwa kiasi flani, na kwa kuwa mashabiki wengi hawajashitukia kudai haki yao, basi unakuwa ‘Unyonyaji uliohalalishwa’ kwa kupoozwa na neno ‘alishangiliwa sana, alifunika sana.
Wasanii wanaofanya hivyo kwa kisingizio chochote, na mnalipwa vizuri na mnatangaza, kumbukeni kauli ya Bob Marley, “You can fool all the people for sometimes, but you can’t fool all the people all the time.”
Badilika, fight for excellence, sio kwa mazoea na kuiga mfano wa aliyekosea hata kama ni msanii kutoka mwezini.
source:Josefly Muhozi
Mwimbaji wa nyimbo za injili toka nchini Nigeria  ajulikanaye  kwa  jina  la  Maheeda  amejikuta  akitengwa  na  kanisa  baada  ya  picha  zake  za  uchi  kuvuja….

Taarifa  zinadai  kwamba kabla  ya  kuanza  kuimba  nyimbo  za  dini, mrembo  huyo  alikuwa  akijihusisha  na  mziki  wa  kidunia ambao  kwa  tanzania  unajulikana  kwa  jina  la  Bongo Fleva


MKALI wa songi linalotamba runingani na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.



Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.

Diamond alisema kuwa, Wema ndiye aliyetangulia kwenda China ambapo yeye aliungana naye siku kadhaa baadaye akitokea kwenye shoo nchini Malaysia.

SIRI YA KWANZA
Akianika siri za kujikuta mikononi mwa mwigizaji huyo mwenye mashabiki wengi zaidi katika tasnia ya filamu za Kibongo, Diamond alisema kwanza ni ukarimu aliopewa na mrembo huyo.

Alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.

“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.

Akaongeza: “Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.


“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.”

SIRI YA PILI
Diamond alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘klasiki’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.

SIRI YA TATU
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’.

SIRI YA NNE
Alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye. 

SIRI YA TANO
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.

HAKUNA CHA FILAMU
Alipoulizwa juu ya madai kuwa walikuwa wakirekodi filamu, Diamond alifunguka kuwa hakuna cha filamu wala sinema na kama kuna mtu anasubiri filamu atakaa sana.

“Naomba nikiri kuwa kweli zile picha hazikuwa za filamu wala nini bali ndivyo hali halisi ilivyokuwa kati yangu na Wema kule China.


“Pia naomba niseme kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi uliishia China na sasa hivi tumebaki kama kaka na dada na ni ruksa kila mtu kumtumia mwenzie katika kazi mbalimbali kama ataona kuna ulazima wa kufanyika hivyo,” alisema Diamond.


Hii ni mara ya kwanza kwa Diamond au Sukari ya Warembo kukiri kuwa kweli alirudisha penzi lake kwa Wema walipokuwa nchini humo wakijiachia.

PENNY HANA CHAKE?
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Diamond, ukifuatisha simulizi hiyo ya mapenzi kati ya msanii huyo na Wema, ni dhahiri kuwa mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ hana chake kufuatia usaliti huo.


Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.

GPL
JESHI la Polisi nchini limewafukuza kazi askari wake 56 katika kipindi cha mwaka mmoja, kutokana na makosa ya kuomba na kupokea rushwa pamoja na utovu wa nidhamu.
  


Kamishna msaidizi wa jeshi hilo, Patrick Byatao, alisema hayo jana alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali hususan masuala ya nidhamu kwa askari wake katika warsha ya siku maalumu ya polisi iliyofanyika mjini Bukoba.
  
Alisema kuwa askari waliofukuzwa ni kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao wamekutwa na tuhuma za utovu wa nidhamu ikiwemo kuomba rushwa kwa wananchi. Kwa kipindi cha mwaka 2012, waliwafukuza askari 35 na mwaka huu 21.
  
Kwa mujibu wa Byatao, wapo baadhi ya askari ambao wamekuwa wakitoa visingizio vya kuomba rushwa kwa sababu mishahara yao ni midogo na haitoshelezi mahitaji yao.
  
Alisema ni heri askari wa aina hiyo wakaacha jeshi, vinginevyo wataendelea kuchukuliwa hatua kama hawatafuata masharti ya kazi yao.

Akitoa mada juu ya kuimarisha maadili ndani ya jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka makao makuu, Andrew Makungu, alisema wameanzisha mkakakati wa kudhibiti vitendo vya ukiukwaji maadili kwa askari wake ikiwemo rushwa.
  
Alitaja maeneo lengwa kuwa ni chumba cha kupokea taarifa za mashitaka, usalama barabarani na upelelezi wa makosa ya jinai. Bado juhudi zinaendelea ili kuboresha maeneo mengine.
  
Makungu alisema ubia wa kiutendaji wa jeshi hilo umekuwa ukiimarika kila siku baada ya sehemu kubwa ya jamii kutambua nafasi yao katika jukumu hilo. 
  
Alisema mambo hayo yanaonekana kutokana na wananchi kufanya ulinzi wa maeneo yao, kuchangia rasilimali kwa jeshi, kutoa taarifa sahihi za uhalifu, kujenga vituo vya polisi na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi. Hadi sasa viko vikundi 5,344 nchi nzima huku Mkoa wa Kagera ukiwa na 431.
  

Naye mgeni rasmi katika warsha hiyo, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, alisema kuwa Jeshi la Polisi limekuja na mkakati wa polisi jamii/ulinzi shirikishi unaoelekeza kuwapo kwa mashauriano, majadiliano ya kiutendaji yanayosisitiza uwepo wa maadili katika kazi, ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa ndani ya jamii.

Chuo cha st.John's pale Dodoma kuna tatizo kubwa la walimu kuwakamata wananfunzi na kuwalazimisha ngono.



Nimeshuhudia mwanafunzi last week amekamatwa na mwalimu kamwambia