advert

http://

Thursday 3 October 2013

MTOTO WA MIAKA 13 AJIFUNGUA MTOTO WA MIEZI 6 SEBULENI BILA KUJIJUA.

MSICHANA aliyejitambulisha kwa jina la Salma Hemedi (13) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Dar amejifungua  maiti ya kichanga cha miezi 6 bila mwenyewe kujijua.
Tukio hilo lilitokea Septemba 25, mwaka huu maeneo ya Ubungo National Housing jijini Dar ambapo asubuhi ya siku hiyo, Salma alilalamikia maumivu ya tumbo lake kiasi cha mama yake aliyejitambulisha kwa jina la Rahma Shabani kwenda kuomba msaada wa kitabibu.

Mwanamke huyo alieleza kwamba baada ya kurudi ndani alikomuacha mwanaye, alimkuta akiwa amejifungua kichanga sebuleni, kitu ambacho hakukitarajia kwa kuwa alizoea kumnunulia vifaa vya kujisitiri wakati wa hedhi kila alipomlalamikia maumivu ya tumbo akijua yupo kwenye siku zake.

Akiwa na manesi walioongozana naye, walimsaidia Salma huku kila mtu akiwa amepigwa na butwaa kwa kilichotokea kwani hakuna aliyekuwa anajua kama Salma alikuwa na ujauzito.

Akiongea na waandishi wetu, Salma alisema alipewa ujauzito na mwanaume aliyemtaja kwa jina la John Vicent ambaye alikuwa mtoto wa mwenye nyumba wao wa zamani.

Salma alisema kuwa John alikuwa akimshawishi kila mara kufanya mapenzi japo alimkatalia kwa kuwa alijua akifanya kitendo hicho atapata mimba.

Salma alizidi kutiririka kuwa John alikuwa akimpa dawa alizodai ni za kuzuia ujauzito.

Baada ya kupata taarifa hizo mama wa Salma pamoja na ndugu zake walitoa taarifa Kituo cha Polisi Urafiki ambapo walifungua jalada la mashtaka lenye namba RB, URP/RB/7316/2013 KUBAKA na kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na uthibitisho wa daktari.

Walimu wa shule anayosoma Salma, walipigwa na butwaa baada ya kupata taarifa hizo na kueleza kwamba hawakuwa na taarifa kwamba denti huyo alikuwa mjamzito.

ZAIDI ya wanafunzi 50 waliochaguliwa kujiunga  katika vyuo vikuu mbalimbali nchini kwa mwaka huu, jana waliandamana kwenda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa lengo la kukutana na Waziri Shukuru Kawambwa, baada ya kukosa mikopo.

Wakizungumza na mwandishi wetu, wanafunzi hao walisema zaidi ya wanafunzi 200  wenye sifa za kupewa mikopo ya elimu na Bodi ya Mikopo (HELBS), wamenyimwa bila maelezo.

Walisema kuwa tangu mwisho wa wiki wamekuwa wakihangaika kujua sababu za kutopewa mikopo kutoka katika bodi hiyo bila mafanikio.

Mwanafunzi Ayoub Suleiman aliyechaguliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alisema kuwa wameamua kumfuata Waziri Kawambwa ili wajue ni kwa nini hawajapewa mikopo hiyo.

Alisema majibu ya wanafunzi walioomba mikopo hiyo yalitoka Septemba 27 mwaka huu, miongoni mwao hawakuwepo kwa maelezo kuwa bajeti imekwisha.

“Waliotupa majibu haya ni wafanyakazi wa mapokezi na walinzi pale bodi ya mikopo, sio wahusika wenyewe kwa kuwa kila tulipoomba kukutana na mkurugenzi, hatukupata nafasi hiyo,” alisema Suleiman.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Godwin Uledi, alisema kuwa juzi waliwashuhudia baadhi ya wazazi wakiwa na suti  na magari ya kifahari wakifika kwenye ofisi za bodi hiyo na watoto wao, na kuingia moja kwa moja kuonana na watendaji, walipotoka walikuwa wakitabasamu, hali iliyoonyesha kuwa wamefanikiwa.

Alisema, wanataka wapewe sababu kwa nini hawajapewa mikopo ilhali wenzao wenye vigezo kama vyao wamepata?

“Taasisi ya vyuo vikuu nchini ‘TCU’ ilitoa mwongozo kuwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu wakiomba vitivo vya elimu, uhandisi, udaktari, kilimo na sayansi watapata kipaumbele katika mikopo, hivyo nasi tulifuata mwongozo huo ili tupewe mikopo lakini hatujafanikiwa.

“Isingekuwa tunahitaji mikopo hii tungeomba katika maeneo mengine ambayo tulikuwa tukikidhi vigezo. Tumeomba katika vitivo hivi ili tupate mikopo,” alisema.

Kwa upande wake mwanafunzi aliyechaguliwa katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Revocatus Baltazary, alisema kuwa wamefungua chuo tokea Septemba 18, lakini ameshindwa kuripoti kutokana na wazazi wake kuwa na kipato cha chini.

“Sasa sina hata kianzio cha kwendea huko, kwa kuwa wazazi wangu hawana uwezo nitakwendaje?,” alihoji.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ntambi Bunyazu, alisema kuwa wizara imewasiliana na bodi ya mikopo, kwamba wanafunzi hao warudi kule wakapewe maelezo zaidi kwa kuwa kila mmoja ana tatizo lake.

Hadi mwandishi wetu  anaondoka katika maeneo hayo, wanafunzi hao waliambiwa waorodheshe tena majina ili wizara iyapeleke HELBS, baada ya wiki moja watakuwa wamepata majibu.

Jitihada za kumtafuta Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HELBS, Cosmas Mwaisobya, kwa ajili ya ufafanuzi wa suala hilo, ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita kwa muda mrefu bila majibu

Leo nimekabidhi madawati 120 Kata ya Manzese kwa shule tatu za msingi fedha kutoka katika mfuko wa jimbo. Bado kuna upungufu wa madawati 570 ambapo dawati moja linagharimu Tsh. 80,000 hadi 100,000.


Binafsi nachangia asilimia 20 ya kila mshahara wangu kuboresha Elimu ndani ya Jimbo la Ubungo!

Ungana nami tuboreshe elimu na kuimarisha pia maabara kwa kuchangia kupitia MPesa 350350.

Pamoja Tunaweza.

Waswahili husema, ‘nyumba ni choo’, wakiwa na maana kuwa nyumba haiwezi kuwa kamili bila kuwa na huduma hiyo ya choo.


Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa choo, lakini si kila nyumba iliyo na choo au hata zile ambazo zina huduma hiyo, basi vyoo ni vibovu, havina hadhi. Zipo aina mbalimbali za vyoo kwa matumizi ya binadamu katika maisha yake ya kawaida.


Vyoo vina matumizi mengi ingawa bado watu wengi hasa katika nchi maskini na zinazoendelea ikiwamo Tanzania wanatumia choo cha kuchuchumaa wakati wa kujisaidia, lakini mijini na katika nchi zilizoendelea, wao hutumia vyoo vya kukaa.

Nyumba nyingi mijini na ofisi mbalimbali zinazojengwa hivi sasa, huwekewa vyoo vya kukaa. Hata zile za zamani zinakarabatiwa na kubadilishwa kwa kuwekewa hivi ambavyo vinaonekana vya ‘kisasa’.
Mgunduzi wa vyoo vya aina hii, Thomas Crapper anasema kwa mtazamo wake aliona kukaa wakati wa kujisaidia ni utambulisho wa ustaarabu na maendeleo.


Hata hivyo, madaktari wanapingana naye wakisema kujisaidia katika vyoo vya kukaa kuna madhara kiafya kwa kuwa mkao huo unaweza kuleta matokeo mbalimbali ndani ya mwili.


Utafiti uliofanywa na mtandao wa ‘naturesplatform’ umegundua kuwa matumizi ya choo cha kukaa huweza kusababisha matatizo mbalimbali ikiwemo kansa ya utumbo mkubwa.


Mtaalamu wetu wa afya wa gazeti la MWANANCHI, Samwel Shita anasema, madhara ya vyoo vya kukaa ni makubwa kwani wakati mwingine yanaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa kutokana na haja kubwa kubaki kwa muda mrefu katika utumbo huo.


Shita anasema mtu anapojisaidia haja kubwa katika choo cha kuchuchumaa, kinasaidia haja yote kutoka kwa sababu ya msukumo unaosababishwa na mkao huo.


“Unapokaa unakuwa umekaa katika choo mwili unakuwa umelegea, hivyo inabidi utumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tofauti na unapochuchumaa,” anasema Shita na kuongeza:
“Matatizo huanza hapo, unapojisaidia ukiwa umekaa na kulazimisha kujikamua unaweza kusababisha vimishipa vidogo katika utumbo mpana sehemu ya haja kubwa ya ndani na ya nje kuvimba na maumivu makali husababishwa na ugonjwa unaojulikana kama ‘hemorrhoid,” anasema.


Anasema ‘hemorrhoid’ ni ugonjwa ambao pia huitwa bawasiri. Mgonjwa hupata uvimbe katika njia ya haja kubwa na hivyo kupata maumivu wakati wa kujisaidia na haja yake mara nyingine huambatana na damu.


Aidha, anasema vyoo hivi pia vinaweza kuwa chanzo cha magonjwa yanayotokana na shambukizi katika utumbo mpana, kitaalamu ‘Inflammatory Bowel Disease’.


“Kila binadamu anapaswa kujisaidia na kuhakikisha haja yote imetoka na kwisha kabisa, inapobakia inaweza kusababisha maambukizi katika utumbo mpana kwa kuwa ule ni uchafu wenye mchanganyiko wa vitu vingi,” anasema Shita.


“Haja kubwa inapokuwa tayari imeshajitengeneza inapaswa kutoka yote, kama itabaki kipindi kirefu inaweza pia kuleta uambukizi katika utumbo mkubwa na hata katika kidole tumbo,” anasema Shita.


“Uchafu huu si tu unaweza kusababisha maambukizi, lakini pia unaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa. Wote tunajua kuwa mkusanyiko wa sumu mbalimbali mwilini unakuweka katika hatari ya kupata saratani, hivyo tatizo hili lisipotafutiwa ufumbuzi mapema linaweza kufikia huku,” anasema Shita.


Daktari Berko Sikirov kutoka Misri ambaye alifanyia utafiti matumizi ya vyoo vya kukaa anasema kuwa iwapo mtu ana tatizo la vivimbe vya ‘hemorrhoid’ linaweza kumalizika iwapo ataacha kutumia vyoo vya kukaa.


Hata hivyo, anasisitiza kuwa tatizo hili linaweza kwisha kama litakuwa katika hatua za awali. Kwa wenye tatizo lililokomaa watalazimika kufuata matibabu kulingana na ukubwa wake.


Dk Sikirov anaongeza kuwa mbali na kupata vivimbe, pia mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutokupata choo kwa muda mrefu.


Anabainisha kuwa kitendo cha haja kutoka kidogo na nyingine kubakia husababisha kuganda katika ukuta wa utumbo na zoezi hilo huendelea mpaka kuwa tatizo sugu.


“Haja kubwa huganda katika kuta za utumbo, hali hii huifanya haja izunguke kwa muda mrefu na ndiyo tatizo hili huanzia hapa,” anasema na kuongeza:
“Unapojisaidia ukiwa umekaa, ile njia ya haja kubwa huwa kama imejifunga, inabidi utumie nguvu nyingi sasa ukiwa na tatizo hili la kukosa haja kubwa huifanya itoke kwa uchache zaidi,” anasema Dk Sikirov.


Aidha, anasema kupata haja kubwa mara kwa mara ni muhimu kwa kuwa usipoitoa maana yake inazungusha sumu katika damu jambo ambalo ni hatari kwa afya.


Anaongeza kuwa kutopata haja kubwa ni kichocheo chenye uwezo mkubwa wa kusababisha saratani ya utumbo mkubwa na uambukizi katika kidole tumbo.


Tafsiri ya kitabibu inasema hali ya kukosa haja kubwa ni pale mtu anaposhindwa kuipata angalau mara tatu kwa wiki. Hata hivyo, ili ujue afya yako ni njema unapaswa kuwa unapata haja kubwa angalau mara moja kila siku.
Daktari Denis Burkitt aliwahi kuandika kitabu cha maelekezo ya chakula ili kuepuka ugonjwa wa saratani. Katika kitabu hicho alieleza namna ambavyo watu wanaweza kujikinga na saratani za aina mbalimbali.


Akizungumzia saratani ya utumbo mpana pamoja na kuelezea vyakula na aina ya maisha, pia aliwaasa watu kutumia choo cha kukaa ili kujiepusha na tatizo hilo.


Anaeleza kuwa kwa Marekani pekee, watu zaidi ya 150,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa.


Mtaalamu wa Ngozi katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Kisali Pallangyo anasema matumizi ya vyoo hivyo yanaweza kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa ya ngozi. Profesa Pallangyo anasema ni rahisi kuambukizwa magonjwa ya ngono na ngozi kwa urahisi pale unapotumia vyoo vya kukaa tofauti na vile vya kuchuchumaa.


Aidha, anayataja magonjwa yanayoweza kuwambukizwa kwa kutumia vyoo vya kukaa kuwa ni kaswende, harara, mba, kisonono, upele na mengine.


“Mtu mwenye magonjwa ya ngozi au ya ngono, anaweza kuyaacha katika ‘sink’ anapolikalia, hivyo ni rahisi kwa mtu mwingine ‘kuyachukua’ mara atakapokaa wakati wa kujisaidia,” anasema Prof Pallangyo.


Anasema vyoo hivi ni hatari kwa afya hasa pale vinapotumika katika jumuiya na kuongeza kuwa ni bora kutumia vile vya kukaa ili kujikinga na magonjwa.
Source: MWANANCHI


Kwa jina unaweza muita Leilani Franco  ana urahia wa nchi mbili (Uingereza / Philippines) alisafiri katika nafasi backbend umbali wa 20m  katika muda wa 10.05 dk katika  tamasha la Royal Hall mjini London Uingereza, tarehe 11 Machi 2013. Backbend binadamu ambaye ana uwezo wa kutembealea mikono na miguu kwa umbali mrefu.


Pia kama inavyothaniwa kwa kawaida Mtu anaweza tumia mikono kwa kulia chakula na kufanya shughuli nyingine, lakini kwa mwanamke huyu imekuwa ni tofauti kabisa, Mwamake huyu ana uwezo wa kutumia miguu yake  katika shughuli zake binafsi kama Kula na kadhalika.....
Hatimaye, Leilani pia anashikilia rekodi ya Dunia kutokana na uwezo wake katika kuuzungusha  Mwili wake. 




TAZAMA MAAJABU YA HUYU MREMBO KATIKA VIDEO!!
Anasema yeye mwenyewe binafsi katika kazi zake za ujasiriamali mtaji wake ameupata kwa kuhongwa na mpenzi wake akachanganya na fedha yake na maisha yanakwenda.


Anafafanua kuwa siku zote mpenzi wako hawezi kuacha kukuhonga kwakuwa kwenye mapenzi kusaidiana ni lazima,kwahiyo haoni ajabu yoyote mtu kuhongwa.

"Kusema ukweli mimi mwenyewe boy friend wangu kanisaidia sana na bado anaendelea kunisaidia,mimi sijali mtu aseme lolote analotaka lakini kama nahongwa for benefit sina tatizo na hilo"alisema Linah.

Ameongeza kuwa tatizo watu wamekuwa wana maneno maneno sana na kufuatilia ya watu badala ya kufanya mambo yao lakini ili mradi mambo yake yanakwenda safi hajali lolote anatazama maisha yake zaidi.

 Mwanalizombe Studios Ni Recording Lebel Inayomilikiwa na Rapper Profesa Jay, Studio ipo msasani na Ameamua kuipa Jina la Mwanalizomba kwasababu Jay Ni mtu wa Ruvuma na Mwanalizombe maana yake ni Mwana Ruvuma na kufanya hivyo ameonyesha mapenzi ya mkoa wake wa Ruvuma. Producer kwenye studio hii ni Duke Touchez.


 Profesa ameshindwa kusema amewekeza kiasi gani cha fedha kwenye studio hio ila fahamu kuwa vifaa vilinunuliwa kwa wakati tofauti na ni vifaa vya hali ya juu sana.



Rapper Prezzo wa Kenya aliyehusishwa hivi karibuni na msako wa polici baada ya kusemekana alirushiana risasi na askari, Prezzo amejitokeza na kuweka mambo wazi kuhusu issue hizo na nini hasa kilitokea siku hio na kuhakikisha jina lake linasafishwa. Prezzo ni moja ya rappers wenye aka ya Bad Boy so sio issue mpya kusikia story kama hizi.



Sasa Bwana Jackson Makini aka Prezzo ana habari mpya kwa shabiki wake kuhusu muziki wake. Kaa tayari kwa ngoma mpya kutoka kwa Prezzo Itaitwa " 7 Am" na itatoka siku yoyote mwezi huu. Star huyu kwa sasa bado anatamba na wimbo wake wa ‘Celebration Of Life’aliyomshirikisha Chess .

Rita Paulsen aka Madam Rita wa Bongo Star Search na Walter Chilambo tayari wameshazijibu Salamu za Nay wa Mitego na jana ilikuwa zamu ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe .

Kwake mbunge huyo, Nay ni msanii wa pili wa Hip Hop anayemkubali zaidi Tanzania baada ya Roma na kwamba anakiheshimu kile alichokisema kwenye wimbo huo kwakuwa ni kazi ya sanaa.

Tazama tweets hizi.



CarolNdosi @CarolNdosi
I wonder if @zittokabwe  ever listens to hip hop..local or international..



@CarolNdosi: I wonder if @zittokabwe ever listens to hip hop..local or international..” I do. Roma is my favourite followed by Ney
@zittokabwe @CarolNdosi surprising, after everything Nay Wamitego said in his new truck Salam zao ft Neiba Hon: Zitto still ranks him his n2


@SadiqAbdallah @CarolNdosi Ney amefanya sanaa. Nachukua maneno yake kama changamoto. Ni kazi ya Sanaa ninayoithamini sana.


 Leo tar 2|10 STARBOY was born... el presidente Diamond Platinumz beibb... ikisemekana Penny na Diamond wameachana lakini Penny alivunja ukimya baada ya kupost huo ujumbe on Instagram.

Pichani juu ni taswira mbalimbali za muonekano mpya wa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye kwa sasa yupo uraiani baada ya kufutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), jana alitikisa Jiji la Arusha baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumfutia kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili.


Lema alidaiwa kutoa kauli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alienda kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha kama anaenda kwenye sherehe za kuaga mtoto wa kike “send off”.
  
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Devota Msofe baada ya wakili wa serikali, Eliananyi Njiro, kutumia kifungu cha 20 kifungu kidogo cha 1 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kuliondoa shauri hilo ambalo lilikuwa lianze kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo. Upande wa serikali ulipanga kuleta mashahidi tisa.
  
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliofurika mahakamani hapo kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo waliupokea uamuzi huo kwa shangwe kubwa.
  
Akizungumza nje ya mahakama mara baada ya uamuzi huo, Lema alisema kuwa alikuwa anajua shauri hilo ni la kutengenezwa ndiyo maana mashahidi wengi walikuwa ni polisi.
  
“Ni kama nimeshinda kesi, na Mungu ameendelea kutupigania, na tutaendelea kupambana kutafuta haki bila hofu maana miili yetu na nafsi zetu zimeishapoteza maumivu kwa sababu ya mateso yaliyojaa uongo na hila.
“Tutaendelea na kelele zetu za kupigania haki bila kurudi nyuma huku uvumilivu ukiwa nguzo yetu kubwa,” alisema Lema.
  
Hata hivyo, alikiri kutamka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mulongo alienda Chuo cha Uhasibu kama anaeenda kwenye “send-off” kwani yeye ndiye alimpigia simu akimtaka afike kusikiliza kero za wanachuo, lakini hakulipa uzito unaostahili suala hilo hasa ikizingatiwa kuwa pale kuna mwanachuo alikuwa amepoteza maisha.
  
Lema alisema kuwa wanaweza kuwa wamemfutia kesi hiyo ili kesho wamfungulie nyingine jambo alilodai kuwa yuko tayari kwani anaelewa kuwa lengo ni kutaka kumuogopesha ili aache kuwatetea wananchi kitu alichodai kuwa hawatafanikiwa kwani tayari ana ganzi mwilini mwake, hivyo haogopi kufa, kesi wala kufungwa.
  
Kwa upande wake wakili wa Lema, Method Kimomogoro alisema kuwa ni vema kama serikali ingeamua kutumia busara ya kuona hakuna kesi toka awali, hivyo wasingefungua kabisa shauri hilo lililopoteza muda wa mahakama na mteja wake, kwani hata maelezo ya kesi yalionyesha dhahiri hakukuwa na kosa la uchochezi.
  
Alisema kuwa sheria inaruhusu kumfurahia, kumkejeli au kumzomea mtu, ndiyo maana hata bungeni wanaonekana waheshimiwa wakizomeana na kurushiana vijembe, na akadai hata kauli iliyodaiwa kutolewa na Lema dhidi ya mkuu wa mkoa ilikuwa kijembe tu.
  
Kimomogoro alilitaka Jeshi la Polisi kutenda kazi zao kwa mujibu wa sheria, huku akiwataka warudi kwenye hoja ya msingi na wawaeleze wananchi endapo wameshawakamata waliohusika na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha.
  
Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mnamo Aprili 24, mwaka huu, mshtakiwa Lema akiwa eneo la Freedom Square ndani ya Chuo cha Uhasibu, alitoa maneno ya uchochezi yaliyosababisha uvunjifu wa amani.
  
Maneno hayo yanayodaiwa kutamkwa ni kinyume na kifungu cha 390 sura ya 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu, marejeo ya mwaka 2002 .
  
“RC anakuja (Chuo cha Uhasibu) kama anaenda kwenye send-off, hajui chuo kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho... (RC) Ameshindwa hata kuwapa (wanafunzi) pole kwa kufiwa na amesema hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu.” Yalinukuliwa baadhi ya maneno yaliyodaiwa kuwa yalitamkwa na Lema.
  
Kauli hizo zinadaiwa zilipandisha hasira za wanafunzi ambao walianza kumrushia mawe na chupa Mkuu wa Mkoa, Mulongo alipokuwa akiwahutubia kuhusiana na tukio la kifo cha mwanafunzi, Henry Koga kilichotokea Aprili 23, mwaka huu.

Kwa miaka mingi Coca cola imekuwa ni bidhaa namba moja yenye ubora wa kimataifa lakini mwaka huu Bidhaa Apple ikiwemo simu za Iphone imechukua namba moja kwa kuwa ni bidhaa boraDuniani.


Namba mbili imechukuliwa na Google kwa bidhaa zake mbali mbali...Namba tatu ndio imechukua Coca Cola


From New York Times 
Apple is the new most valuable brand in the world, according to a closely followed annual report. The report, to be released next Monday, is from Interbrand, a corporate identity and brand consulting company owned by the Omnicom Group that has been compiling what it calls the Best Global Brands report since 2000. The previous No. 1 brand, Coca-Cola, fell to No. 3.
Not only has Apple replaced Coca-Cola as first among the 100 most valuable brands based on criteria that include financial performance, this is the first time that the soft drink known for slogans like “It’s the real thing” has not been No. 1.