advert

http://

Tuesday 2 July 2013

ZIARA YA RAIS OBAMA NCHINI YAMALIZIKA LEO





 Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili iliyoanza jana.Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walitembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo. 

PICHA ZAIDI ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO



NHIF YATOA NGAO KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA TIKA


Naibu Waziri wa Elimu katika Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Kassim Majaliwa akikabidhi ngao iliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa mshindi wa mashindano ya TIKA yaliyofanyika mjini Morogoro kwa Kiongozi wa timu ya Garage FC Jumanne Wida baada ya kuibuka washindi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba akikabidhi ngao kwa Shaaban Mrisho kwa kuibuka washindi katika mashindano ya TIKA yaliyodhaminiwa na NHIF.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akipeana mkono wa pongezi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera baada ya kupokea cheti cha ushiriki na mchango wa NHIF uliotolewa kufanikisha maadhimisho ya Serikali za Mtaa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akionesha cheti kilichotambua mchango wa NHIF katika maadhimisho hayo.
Kikosi cha Timu ya Garage FC ambacho kiliibuka mshindi katika mashindano ya TIKA wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Mfuko uliodhamini mashindano hayo.



MKUTANO MKUU WA TANO WA WADAU WA MFUKO WA GEPF WAFANA MJINI ARUSHA




Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akifungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daudi Msangi akifafanua jambo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa tano wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), jijini Arusha.
 Mkurugenzi Masoko na Uendeshaji wa GEPF, Anselim Peter akitoa mada.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Wiliam Erio akifuatilia mada wakati wa mkutano huo. 
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akimsikili kwa makini Meneja Masoko na Utekeleza wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukamazina mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha. 



WINDHOEK SABA SABA PAVILION


Come visit our completely renovated Windhoek Pavilion & VIP Lounge! Air conditioning, restrooms, a new stage & sound system added for 2013! Arrive early and beat the traffic, as this pavilion opens an hour before everyone and stays open until late. The Windhoek Pavilion is the only place to offer your favorite beer along with shows & entertainment, giant screen, pool tables and a VIP lounge all in a truelly premium setting. Watch out for the Green Party we are hosting this weekend!!!
Traditional dancers, acrobats and so much more exciting entertainment exclusively at the Windhoek Pavilion...
Our friendly Windhoek Hostesses are an elite team of premium hostesses whose job is to welcome, delight, and help co-ordinate our visitors in our super premium pavilion. Please be sure to visit us and experience the only 100% PURE BEER in Tanzania.



MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL AFUNGA MKUTANO WA SIKU TATU WA VIONGOZI WA KIMATAIFA WENYE LENGO LA KUTOKOMEZA NJAA BARANI AFRIKA,JIJINI ADDIS ABABA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mommmed Gharib Bilal, akifunga Mkutano wa siku tatu wa Viongozi wa Kimataifa wenye lengo la kutokomeza njaa Barani Afrika .Mkutano huo ulimazika jana jioni mjini Addis Ababa Ethiopia.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kimataifa kuzungumzi juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika uliomalizika mjini Addis Ababa Ethiopia leo.
Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal wakifuatilia kwa makini mkutano wa Afrika uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika . Mkutano huo ulimalizika jana jioni July 01-2013 mjini Addis Ababa Ethiopia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Viongozi wa kimataifa waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia July 01-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mommmed Gharib Bilal na ujumbe wake, wakiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa Viongozi wa kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika . Mkutano huo ulimalizika jana jioni mjini Addis Ababa Ethiopia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwenyekiti wa AUC Dk. Nkosazana Dlamina Zuma, kwenye ukumbi wa Mikutano wa umoja huo baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Viongozi wa Kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia jana jioni July 01-2013.(Picha na OMR).








MAPOKEZI YA RAIS OBAMA IKULU, NA MKUTANO WAKE NA WANAHABARI JIJINI DAR LEO


Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam mchana wa leo.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mgeni wake,Rais Barack Obama wa Marekani wakati walipokuwa wakielekea sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Waandishi wa habari Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakizungumza na waandishi wahabari Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.PICHA NA ISSA MICHUZI,IKULU.



TRENI YA MWAKYEMBE JIJINI DAR YAGONGWA LEO,KUTOTOA HUDUMA KESHO


Leo mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili ovya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika.

Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la Kamata. Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo la daladala ambapo majeruhi  wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli  mmojawapo akiwa  mahututi.

Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini  kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo  jioni Julai 01, 2013, imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasiri. 

mabadiliko haya yamebidi yafanyike   kufuatia Jiji la Dar es Salaam kuwa na hekaheka ya kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama.

Aidha uongozi wa  TRL unawataarifu wakazi wa jiji kuwa kesho Julai 02, 2013, huduma za treni ya jiji hazitakuwepo hadi keshokutwa Julai 03, 2013, ambapo zitaendelea kama kawaida.

Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
 Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.

Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.



MASANJA, SHILOLE WAFIKA ULIPO MJENGO WA UBALOZI WA TANZANIA MAREKANI


 Juu na chini ni Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakiwa nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC mara walipopita na kupiga picha nje ya mjengo Jumapili June 30, 2013 walipokua wakitokea uwanja wandege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Kesho mchana Jumanne April 2, 2013 watatembelea rasmi mjengo huo na kusaini kitabu cha wageni.
 Masanja na Shilole wakiwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wakiangalia menyu tayari kwa kuagiza dinner ya mchana walipokwenda mgahawa wa kijiji cha Swahili uliopo Beltsville, Maryland
 Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na mmiliki wa mgahawa wa Swahili Village Bwn.Kelvin.
Masanja na Shilole wakiingia kwenye usafiri wao kuelekea Hotelini walikofikia.


WASANII WA TAMASHA LA FILAMU GRAND MALT WATOA MSAADA WA VYANDARUA HOSPITALI YA SEKOU-TOURE LEO JIJINI MWANZA.


 Picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
 Sehemu ya vyandarua vilivyotolewa msaada vikiwa tayari vimefungwa na wasanii wa filamu hapa nchini,mara baada ya kutoa msaada wa vyandarua hivyo ndani ya wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Mkoa wa jiji la Mwanza-Sekou-toure  mapema leo asubuhi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt..
 Msanii wa Bongo Movie,Jacline Wolper akiwa katika wodi ya wazazi ,Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekou-toure akifunga chandarua kwenye moja ya vitanda hospitalini hapo,ikiwa ni sehemu ya vyandarua vilivyotolewa na wasanii hao kupitia kinywaji cha Grandmalt
 Wasanii Irine Uwoya na Shamsa Ford wakiwa na mmoja wazazi akiwa amembeba mtoto aliezaliwa kwenye hospitali hiyo ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-toure  mara baada ya wasanii hao kutembelea Hospitali hiyo na kutoa vyandarua kwenye wodi Wazazi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza,Halifa Hassan Hida akizungumza machache (mbele ya wasanii wa Bongo Movie (hawapo pichani) ikiwemo na kuwashukuru wasanii hao wa filamu kwa kitendo cha kiungwana kabisa katika suala zima la kuisaidia jamii yao inayowazunguka kwa njia moja ama nyingine na pia amewataka kuwasaidia wasanii wachanga wa jiji la Mwanza na kuwaelekeza njia sahihi za mafanikio katika tasnia hiyo ambayo kwa sasa imezidi kushika kasi siku siku. 
 Meneja wa kinywaji cha Grandmalt Consolata Adam akipokea mkono wa shukurani  kutoka kwa katibu wa Afya hospitali ya Sekou-toure Bwa.Daniel Temba,mara baada ya kabidhi msaada wa vyandarua sanjari na wasanii mbalimbali wa filamu,makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure,ikiwa ni sehemu ya wasanii hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Wasanii mbalimbali wakiongozwa na Raymond Kigosi  wakikabidhi msaada wa vyandarua kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure, kwa katibu wa afya wa Hospitali  hiyo Bwa.Daniel Temba ikiwa ni sehemu ya wasanii hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
 wasanii wakiendelea na zoezi la  wakikabidhi msaada wa vyandarua kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure kwa katibu wa afya wa Hospitali  hiyo ikiwa ni sehemu ya wasanii hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye  uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
 Baadhi ya wasanii wa Filamu hapa nchini a.k.a Bongo Movie Unity wakiwasili kwenye hospitali ya Sekou-toure tayari kwa kushiriki zoezi la kugawa vyandarua kwenye wodi ya wazazi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha GrandMalt mapema leo asubuhi.
 Mlezi wa Bongo Movie Unity,Jacob Steven a.k.a JB a.k.a Bonge la Bwana wakisalimiana na Afisa mhausiano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza,Bwa.Joseph Mlinzi,pichani kati ni msanii wa filamu Singo Mtambalike.
 Baadhi ya Wasanii hao wa Bongo Movie Unit wakitoka kwenye wodi ya Wazazi mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua vilivyotolewa kwa hisani kubwa ya kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt.




RAIS BARACK OBAMA AWASILI NCHINI MCHANA HUU


 Rais Barack Obama wa nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto zao,wakiwasili chana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mchana wa leo. Kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.nyuma ya Rais na mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama.
Rais Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Rais Barrack Obama katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
RaisDkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwaongoza wageni wao Rais Barrack Obama wa Marekani na mkewe Michelle kuangalia ngoma mbalimbali za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ziara ya siku mbili nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani wakifurahia na kufuata mapigo ya ngoma za utamaduni katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu jijini Dar es Salaam leo mchana wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo wa Marekani na ujumbe wake.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwatambulisha baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kwa Rais Barrack Obama na mkewe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha na Freddy Maro,Ikulu.