advert

http://

Tuesday 15 October 2013

ZITTO KABWE ATIMIZA AHADI YAKE,ATAJA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa sh milioni 384 kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi.

Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu, aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.
  
Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
  
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya nchi.
  
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi licha ya kuhudumiwa kila kitu na serikali.
  
Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
  
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini,” alisema Zitto.
  
Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka 1998.
  
Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na biashara huru.
  
“Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi wa uchuuzi badala ya uzalishaji,” alisema.
  
Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo kujua wataendeleza vipi.
  
Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi, na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa Watanzania.
  
Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi ya jamii kwa wakulima akisema imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa kuhakikisha wanaongeza Watanzania wenye hifadhi ya jamii kwa kuanza mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for social security to small holder farmers).
  
“Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia uwekaji akiba katika nchi na kuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.
  
“Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yangu ya Hesebu za Serikali (PAC) itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini,” alisema.
  
Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribani sh bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua fedha zinatumika namna gani.
  
Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana. Kwamba wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini.

Tanzania  Daima 

Tukiwa tunakumbuka na kusherekea maisha ya Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, unaweza kuangalia hii documentary inayohusu maisha ya mwalimu kuanzia alipozaliwa hadi alipoanza harakati za siasa.

Siku kama ya leo natumaini  haya yatakuwa material mazuri kwa ajili yako. enjoy.

Sasa nani zaidi?SIKILIZA KWANZA HAPA CHINI!!

Mwili wa mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja ukining'inia juu ya mti.

 Mwanaume huyu amekutwa amejinyonga usiku wa kuamkia juzi mjini Morogoro. Chanzo cha mtuhuyu kujinyonga hakijafahamika. Kwa mujibu wa askari aliyekuwepo eneo la tukio alidai kwamba askari wa doria waliokatiza kwenye eneo hilo majira ya saa 10 usiku walishuhudia mwili wa mtu huyo ukining'inia juu ya mtu.
 Askari akipanda juu ya mti kwa ajili ya kuushusha mwili wa marehemu.

Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari

SOURCE:http://www.bossngasa.com/2013/10/akutwa-amejinyonga-kwenye-mti-mkoani.html#more

TOFAUTI na inavyoaminika na wengi kuwa watumishi wa Mungu ni watu safi, safari hii Mchungaji Obed Ntimba wa Kanisa la Anglikana Gongo la Mboto, Dar es Salaam amejikuta akivunja agano la Muumba baada ya kunaswa gesti akiwa na mke wa mtu.

 Tukio hilo la aibu lilimkuta mchungaji huyo Ijumaa iliyopita saa saba na nusu za mchana katika gesti moja (jina lipo) iliyopo nyuma ya Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar.
  
Siku moja kabla ya tukio, makachero wetu walitonywa kuhusu dhambi hiyo na mtu wa karibu na watu hao akisema kuwa anaumia kwa sababu mchungaji huyo ana mke na watoto na mwanamke huyo, Rose ni mke wa mwanajeshi kwa hiyo aliamini tendo wanalotaka kulifanya ni uovu katika jamii.
  
 Mtoa habari wetu huyo alisema tukio hilo lilipangwa kukamilika kesho yake Ijumaa katika gesti hiyo ndipo kazi ya kuwafuatilia hatua moja baada ya nyingine ilianza.
  
Ijumaa saa sita mchana, mtonyaji wetu alipiga simu  na kuweka wazi kwamba wawili hao wapo njiani kuelekea gesti, kila mmoja kwa usafiri wake.
  
 Ndipo makachero wetu  walipowatonya polisi na kuambatana nao mpaka kwenye gesti hiyo na kujipanga kwa mbinu za kisasa za kutoonwa na ‘adui’.

 Makachero hao  walifanikiwa kupata ramani ya chumba walichoingia wawili hao ambapo ‘rumu’ namba 1B ndiyo iliwasilishwa kwamba Rose na mchungaji wake wamo humo.

Saa saba na nusu mchana, Makachero wetu na polisi waliingia hadi mapokezi ya gesti hiyo kwa kificho na kutoa maelekezo kwa mhudumu. Mhudumu aliongozana nao hadi mlangoni na kugonga lakini haukufunguliwa.
  
 BAADA YA DAKIKA TANO
Wakati mlango huo ukigongwa na mhudumu bila kufunguliwa, mchungaji huyo alisikika akisema na kuuliza:
“Subirini kwanza.”
“Lakini ninyi ni akina nani?”
  
 Baada ya dakika tano kupita, mlango ulifunguliwa, mchungaji akakutana na macho ya timu nzima. Alipigwa butwaa asijue la kufanya huku akitetemeka, Rose alikuwa ndani ya khanga moja!
  
 MCHUNGAJI MSOBEMSOBE HADI POLISI
Polisi waliwabeba msobemsobe wote hadi Kituo cha Polisi cha Urafiki-Ubungo, Dar ambapo kila mmoja alianza kujieleza.
  
 MCHUNGAJI APANGULIA HUDUMA YA KIROHO
Kituoni hapo, Mchungaji Ntimba alipobanwa kuhusu sababu za kuingia gesti na mke wa mtu, alisema waliingia kwa ajili ya huduma ya kiroho kwani mwanamke huyo alikuwa anataka kufungua kanisa ndipo alipomuomba yeye amsaidie.
  
 “Mimi sikuwa na lengo baya jamani. Huyu dada alihitaji kufungua kanisa, akaniambia ili nimshauri hawezi kukaa  sehemu ya wazi kwa kuwa mume wake ni mwanajeshi anaweza kuonekana na watu wakampa taarifa.
  
 “Ndipo nikaamua kwenda naye katika nyumba ile ya kulala wageni kwani wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya huduma, wakitokea nchi mbalimbali huwa wanalala pale na wahusika wa pale wananifahamu sana.
  
 “Baada ya kuingia gesti nilibanwa na haja ndogo, nikaenda kujisaidia. Cha kushangaza niliporudi nilimkuta huyu dada amevua nguo zote na kuanza kunishawishi lakini sikuwa na lengo hilo jamani,” alijitetea mchungaji huyo.

 Baadhi ya picha zilizopo  zinamuonesha mchungaji huyo akiwa amevaa suruali lakini amesahau kufunga zipu huku kondom zikiwa pembeni kitandani!
  
 MSIKIE MKE WA MTU SASA
Baada ya mchungaji kutoa maelezo yake, mke wa mtu naye alianza kutiririka ya kwake huku akionesha ushahidi wa meseji za simu ambazo mchungaji huyo alikuwa akimtumia akimshawishi kumpa penzi.
  
 “Huyu mchungaji nilikwenda kwake kwa lengo la kufanya kazi kanisani lakini kuanzia hapo amekuwa akinishawishi kuwa anataka nimpe penzi ili aweze kuniweka katika sehemu nzuri kanisani.
  
 “Nilikuwa nakataa, lakini akasema tukutane pale gesti tuongee zaidi. Nilikataa kukutana gesti, akaniambia pale ni ofisini, mara nyingi akiwa anaongea na waumini mambo muhimu ya huduma ya kiroho huwa anakutana nao pale.

 “Nikakubali lakini kabla hata hatujaongea chochote alianza kuvua nguo zake na kuanza kunilazimisha tufanye mapenzi huku akiwa na ‘kinga’ kabisa na mimi nikavua nguo lakini kabla hajatimiza lengo lake ndipo wakaingia watu wakiwa na askari.
  
 “Mimi nashukuru sana kwa sababu hawa ndiyo wameniokoa. Nilikuwa nikisikia habari za huyu mchungaji kuwa ana tabia ya kuwafanyia wasichana wengi vitendo hivyo na kweli leo ndiyo nimeamini,” alieleza mwanamke huyo.
  
 Katibu wa kanisa hilo (jina halikupatikana mara moja) alimuombea msamaha mchungaji kwa waandishi huku akionesha kuumizwa na kitendo hicho baada ya kuoneshwa ushahidi na kukiri kwamba una ukweli tofauti na alivyokuwa akifikiria awali kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

-Source: Global Publisher.

MAMA mzazi wa mkali wa ngoma ya Number One, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameingilia kati penzi lililofufuka upya kati ya mwanaye na staa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu.

Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Akizungumza nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.

“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema mzazi huyo.

Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.

“Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.

GPL.

Wiki ilopita kutoka babamzazi.com tulitaka kujua kati 
ya Wema na Lulu nani anakubalika zaidi na hapa chini ni matokeo.
WEMA SEPETU
  49 (52%)
 
LULU MICHAEL
  44 (47%)
 
Votes so far: 93
Poll closed 

Wiki hii ni kati ya DJ Manywele-TBC fm na DJ COBO-Times fm nani zaidi?
Kwa mujibu wa ITV tukio lilitokea saa kumi na mbili na nusu nyumbani alipokua akiishi mama mzazi wa mwandishi wa ITV Ufoo ambae ni Anastazia ambapo baada ya taarifa kufika ITV,
timu ya ITV  ilifatilia tukio hilo na kushuhudia gari la wagonjwa la Hospitali ya Tumbi Kibaha Pwani ikiwa imembeba Ufoo kumuondoa kwenye hospitali hiyo ili kumuwaisha Muhimbili hospital.

Wakati huo mpaka Ufoo anafikishwa hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha dharura, miili miwili ambayo ni wa mama yake mzazi na mwanaume aliemuua mama kwa risasi na kisha kujiua yeye pia kwa risasi ya kichwa ilikua ikiingizwa kuhifadhiwa.

Shuhuda wa tukio hilo ambae ni mpangaji aliepanga nyumba ya mama yake na Ufoo, Mr Ngowi amesema ‘walikua wanagombana huko ndani na kelele za bastola zinasikika, tukafika tukakuta damu zimetapakaa chini barazani tukamuona na mama amelala chini ndio nikatoa taarifa kituo cha polisi na kukuta Marehemu amemuua mama mkwe na yeye mwenyewe kujiua’

Mwenyekiti mtendaji wa IPP Reginald Mengi alifika hospitali kumjulia hali Ufoo ambapo alisema ‘nimesema na Madaktari ana majeraha lakini hatujui ni mangapi kwa sababu bado wanamfanyia uchunguzi na baadae kidogo atafanyiwa upasuaji, nina imani kwamba Ufoo atarudi kwenye hali yake ya afya njema’

Producer wa Fish Crab Studios Lamar yuko kwenye shughuli ndefu ya kutengeneza wimbo wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya Tanzania.

Wimbo huu wenye lengo kuu la kupiga vita Drug Abuse Tanzania utahusisha na kuwa na sauti kumi tofauti za wasanii wa hapa Bongo.

Mpaka sasa wasanii wengine wanaingiza vipande vyao kwenye wimbo huo na kila msanii ana bar nne kwenye wimbo huo so utakuwa na kama dakika 5 na wote watatosha.

Yote Tisa Tayari mdogo wake Diamond ajulikanae kama Dogo S.Kide mtoto wa mama shamte ana wimbo wake uitwao kitale inayousu madawa ya kulevya na kasema ni agizo toka ikulu kwa babu kikwete.Isikilize hapa Chini ni balaa tupu na kama ujumbe imefika.

.