advert

http://

Saturday 8 June 2013

Simu chanzo cha maendeleo, ndoa kusambaratika.



Na Kalunde Jamal, Mwananchi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi katika mikoa mbalimbali nchini umegundua kuwa mbali ya kusambaratisha ndoa nyingi, simu pia zimekuwa adui mkubwa kwa baadhi ya watumiaji badala ya kuwanufaisha kama inavyotakiwa.
Uzuri na ubaya wa simu

Wananchi walieleza uzuri na ubaya wa simu ambapo Peter Tesha mkazi wa Arusha aliitaja simu kuwa ndiyo chanzo cha kumfikisha alipo sasa akikosa fedha za matumizi yake ya kawaida licha ya awali kumiliki miradi mingi iliyokuwa ikimwingizia kipato.
Anaeleza kuwa baada ya kuoa mwaka 2009,
alibahatika kupata watoto wawili na mkewe na maisha yao yakaendelea vizuri huku yeye akiendelea na biashara yake ya maduka matatu aliyokuwa akilimiki jijini Arusha na mawili ya Moshi.
Anasema kuwa katika maisha yake na mkewe hakuwahi kushika simu ya mkewe huyo mbali mkewe kuwa hodari wa kuchunguza simu yake.
Hata hivyo siku moja bila kupanga alichukua simu ya mkewe na kusoma ujumbe mfupi aliotumiwa, jambo analoapa kutolifanya tena maishani mwake kwani alikutana na ujumbe aliouelezea kuwa ulikuwa wa majibizano kati ya mkewe na mwanamume mwingine ambaye hata hivyo jina lililotumika lilikuwa la kijiji badala ya mtu.
“Siwezi kusahau, hata huu umaskini unaoniandama ni madhara ya simu. Ujumbe ule ulikuwa wa kulaumiana kati ya mke wangu na huyo mwanamume kuwa hawa watoto wangu ni wake, mke wangu akiuliza; Kwa nini umewatelekeza na kuniachia mzigo wa kulea mimi ambaye siyo watoto wangu?”anasema Tesha.
Anafafanua kuwa ujumbe huo ulifafanua: “Kama akiendelea kufanya hivyo ataiuzilia mbali nyumba aliyompa kwa ajili ya watoto, ambao mimi siku zote nilikuwa nikiamini ni baba yao.”
Anaeleza kuwa tangu alipofungua simu ya mkewe na kusoma ujumbe huo maisha yake yalibadilika kwani alikwenda kuwapima DNA watoto hao na kumbana mama yao ambapo ilibainika kuwa ni kweli watoto hao sio wake, jambo lililomchanganya na kumtia aibu kwenye familia na jamii hivyo akaamua kuwa mlevi.
Tesha anasema kuwa kuanzia hapo aliacha kusimamia biashara zake kutokana na kuchanganyikiwa na kukwepa aibu, huku akiishi kwa kujificha kwa zaidi ya mwaka na alipotulia na kujifikiria kwa nini amekuwa hivyo alikuwa tayari ameshachelewa, kwa kuwa baadhi ya maduka yalikuwa yamefungwa na aliowaacha hakuwa na cha kuwafanya akibaki na duka moja la Arusha ambalo pia lilikuwa limekufa kutokana na kuwa na bidhaa chache.
“Naishi kwa ushauri na ndiyo maana mara nyingi nimekuwa nakutumia ujumbe wa kutaka unishauri kwa kuwa siiamini tena akili yangu wala mwili wangu. Kama mwanamke ambaye nilikuwa naishi naye miaka yote aliweza kubeba mimba za mtu mwingine na nisijue, sina sababu ya kujiamini tena, nimekuwa masikini kwa sababu ya simu, sitamani simu ya mtu zaidi ya hii yangu, ambayo wakati mwingine huwa naamua kuifunga,”anamaliza Tesha.
Wakati Tesha akieleza hayo, upande mwingine Jennipher Lazaro wa Tanga anasema kuwa hawezi kuishi bila simu kwa kuwa humsaidia mambo mengi ikiwamo kujifunza zaidi kupitia mtandao, kumuunganisha na marafiki walio mbali naye.chanzo/www.babamzazi.com

ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YA MSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE.

Mkurugenzi wa Stoppers Entertainment, Mukhsin Mambo (Mc Stopper) akimvisha Sash Mrembo Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013

Mkurugenzi wa Stoppers Entertainment, Mukhsin Mambo (Mc Stopper) akimvisha Crown Mrembo Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya kuvuliwa taji hilo mrembo Diana Amimo alipodanganya Uraia wake.

Redds Miss Nyamagana 2013/14 Rosemary Peter katika pozz, mara baada ya kutawazwa rasmi kushika taji hilo, katika hafla fupi iliyofanyika katika hotel ya New Mwanza ya kumvua aliyekuwa akishikila taji hilo Mrembo Diana Amimo baada ya kudanganya Urai wake na Umri.

Mkurugenzi wa Club Fusion wadhamini wa shindano la Miss Nyamagana 2013, Mr. George akipeana mkono na Redds Miss Nyamagana 2013 Rosemary Peter, mara baada ya kuvishwa taji hilo.
Taarifa kwa Wadau wote:
ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YA MSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE.
 
Rosemary Peter, ni mshindi wa pili katika shindano la kumtafuta Redds Miss Nyamagana 2013, shindano lililofanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza.
 
Alhamisi ya tarehe 06/06/2013, Rosemary peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo.
 
Udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja mara baada ya shindano hilo.
 
Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24, Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013/14

SSPRA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO WAANDAA SHEREHE YA KUMUAGA PADRI DOKTA CHARLES KITIMA JANA KATIKA UWANJA WA RAILA ODINGA.

Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mt.Augustino Mwanza(SAUT) Mh.Padri Dokta Charles Kitima leo amewaaga wanafunzi na jumuiya yote ya mtakatifu augustino katika kiwanja cha raila odinga na kumkaribisha Makamu Mkuu Mpya Padri Pius Mgeni kuwa ndiye makamu mkuu wa chuo kwa sasa.

Akizungumza katika sherehe hiyo ya kumuaga padri charles kitima awewataka wasomi wote wa vyuo vikuu na viongozi wote kuiga mfumo wa hayati Mwalimu J.K Nyerere ambao aliutumia katika kuiongoza Tanganyika na kuwa mstari wa mbele katika kutetea rasimali za wazawa ambazo utoroshwa kwenda nje kwa njia za panya.

Aidha,Amewataka vijana kuendelea kusoma kazi mbalimbali ambazo Hayati Mwalimu JK Nyerere katika uhai wake aliwahi kuziandika kwa ajili ya watanzania,kama marejeo ya kuondokana na matatizo yanayoikabili la tanzania kwa sasa.

 Katika sherehe hiyo ya kumuaga iliendana sambamba na kikizinduua kitabu kipya kilichoandikwa na Boniphace Pesambili Mgeta ambaye ni mwanafunzi katika shahada ya mwasiliano ya umma(Bachelor of Arts in Mass Communications) katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza.Pia amempongeza boniphace kwa kuandika hicho kitabu na kutaka aendeleze weledi katika kuandika kazi ambazo zinatetea haki za watanzania.

Padri charles kitima ametoa zawadi ya kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha mtakatifu augustino kwa kuwanunulia nakala 300 ya vitabu vilivyoandikwa na Bw. Boniphace Mgeta

Kitabu hicho kimeandikwa kufuatia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi wailosoma katika chuo hicho katika kafuta suluhisho la matatizo mbalimbali ambayo yanawakabiri watanzania kwa sasa.

Zoezi hilo la uzinduzi wa kitabu lilisindikizwa na wakuu wa idara mbalimbali,Idara ya mawasiliano ya umma,Mkuu wa Idara ya sheria,na Mkuu wa idara ya Mahusiano ya jamii na matangazo.
Baadhi ya wanajumui ya  Mt.Augustino wa kimsikliliza Padri Dokta Kitima jana wakati wa kumwaga.

    
Padri Dokta Charles Kitima akitoa hotuba yake kwa wanafunzi na wanajumuiya ya SAUT.





Wa kwanza toka kulia ni Boniphace Mgeta ailiyeandika cha Ufiasadi wa Baadhi ya viongozi wetu wa Nchi