advert

http://

Saturday 11 May 2013

WIGAN YATWAA KOMBE LA FA

Timu ya wigani imechakua kombe la FA baada ya kuichapa man city bao 1-o
bao hiyo limewekwa kinyani na Ben Watson katika dakika ya 90" kabla ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho kuashilia mchezo umekwisha.hivyo man city wameachwa mdomo wazi na hawaamini kilichotokea 

kushoto ni kocha wa wigan akishangilia ushindi na katikati ni wachezaji wa man city wakiangalia jinsi goli lilivyokuwa likingiia kinywani na kulia ben waston akichangilia goli alilofunga.

LAMPPARD AIPA CHELSEA TIKETI YA KUCHEZA UEFA!


Mabao mawili ya Frank Lampard yaliifanya Chelsea kuibuka na ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Aston Villa.

Magoli hayo mawili aliyoyafunga Lampard ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo na timu ya taifa ya Uingereza, yamefanya avunje rekodi ya Bobby Tambling mchezaji wa zamani wa Chelsea na kuweka rekodi mpya ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo ya mashariki mwa London baada ya kufikisha idadi ya kufunga jumla ya mabao 203 tangu aanze kuichezeainazohusiana

Christian Benteke wa Aston Villa na Ramires wa Chelsea walipewa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti.Chelsea walikuwa wageni kwenye uwanja wa Villa Park katika mechi ambayo ilikuwa na ushindani huku kadi mbili nyekundu zikitoka.
Kwa matokeo haya Chelsea sasa wanasalia kwenye nafasi ya tatu na pointi 72 huku Aston Villa wakiwa bado kwenye nafasi ya 13 na pointi 40.
Michezo mingine ya ligi kuu ya England inayofikia tamati wiki ijayo itachezwa kwa nyakati tofauti hapo jumapili.
Stoke City watakuwa wakipambana na Tottenham Hotspurs wakati Everton watakuwa nyumbani kuwakaribisha West Ham United.
Kwingineko Fulham watawakaribisha Liverpool kwenye uwanja wa Craven Cottage huku Norwich wakitarajia kupapatauana na West Brom.
Sunderland wao watakuwa wakicheza mchezo ambao kocha wao Paulo Di Canio ameuita mchezo wa fainali kwao dhidi ya Southampton,mchezo ambao utaamua hatima yao ya kushuka ama kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao.
Mabingwa Manchester United wao watacheza mchezo wao wa mwisho kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya Swansea, mchezo ambao United watautumia kumuaga kocha wao Sir Alex Ferguson aliyetangaza kustaafu msimu ujao na pia watakuwa wakikabidhiwa rasmi kombe la ubingwa wa ligi kuu msimuu huu.
Na mchezo wa mwisho QPR watakuwa wakipambana na Newcastle, mchezo ambao BBC Ulimwengu wa soka itakuwa ikutangazia moja kwa moja kuanzia majira ya saa kumi na moja na nusu jioni kwa saa za Afrika mashariki sawa na saa kumi na nusu Afrika ya kati.
CHANZO BBC SWAHILI.CO.UK

Tutu aacha kuunga mkono ANC


Askofu mstaafu wa Cape Town, Afrika Kuisni, Desmond Tutu, amesema hatapigia kura tena ANC, chama tawala cha nchi hiyo.
Katika makala aliyoandika kwenye magazeti ya Mail na Guardian, Desmond Tutu, aliyepewa tuzo ya Nobel ya amani, alisema ANC iliongoza vema vita vya ukombozi lakini haikufanikiwa kuwa chama cha kisiasa.
Alitoa mfano wa tofauti baina ya maskini na matajiri, fujo na rushwa kuwa sababu zinazomfanya kuacha kuunga mkono chama hicho.
Desmond TutuZamani Desmond Tutu alikuwa mfuasi mkubwa wa chama hicho lakini katika miaka ya karibuni amekilaumu kwamba hakikushughulikia watu wa kawaida.chanzo,www.bbcswahili.co.uk

Moyes:Sikupanga kuondoka Everton


Kocha wa Everton David Moyes ambaye msimu ujao atakuwa kocha mkuu wa Manchester United, amesema hakupanga kuondoka Goodison Park ila ilikuwa vigumu kukataa ofa ya kuifundisha United.

Moyes mwenye umri wa miaka 50 ameyasema hayo wakati akizungumzia mchezo wa siku ya jumapili wa ligi kuu soka nchini England.

Kocha huyo raia wa Scotland amesema kuwa alipanga kuongeza muda wa kuifundisha Everton baada ya kukaa kwa miaka 11, lakini alipopewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha Manchester United alishindwa kukataa.Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya kutangaza rasmi ataicha Everton mwishoni mwa msimu huu na kujiunga Manchester United kama mrithi wa Sir Alex Ferguson ambaye alitangaza kustaafu kufundisha soka baada ya msimu huu kumalizika.
"Sikupanga kuondoka Everton, ila kiukweli ilipokuja ofa ya United, sikuweza kusema hapana" Alisema Moyes ambaye alianza kucheza soka kwenye klabu ya Celtic.
Aidha Moyes ambaye aligoma kujibu chochote kuhusu United, alisema anatambua changamoto atakazokutana nazo hapo jumapili wakati atakapokuwa akiongoza timu yake ya Everton katika mchezo wa ligi kuu England dhidi ya West Ham
Kocha wa Celti, Neil Lennon amepinga uvumi wa kuwa huenda akamrithi Moyes kwenye viunga vya Everton huku Michael Laudrup yeye akisema anataka kuendelea kuifundisha Swansea
CHANZO CHA HABARI.www.bbcswahili.co.uk

RADIO SAUT FM MWANZA YATIMIZA MIAKA 15 TOKEA KUANZISHWA KWAKE




Watangazaji na wafanyakazi wa radio SAUT FM iliopo Mwanza wanayofuraha ya kuwakaribisha wadau na wapenzi wao katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa radio hiyo inayotimiza miaka 15
tokea kuanzishwa kwake  itakayo fanyika kesho Juma mosi kuanzia saa 1 usiku hadi majogoo katika viwanja vya Raila Odinga viliopo katika chuo kikukuu cha Mt. Augustino  jijini Mwanza.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa maandalizi na Mkurugenzi  wa idara ya Burudani radioni hapo Bw. Lucas Maziku kuwa kutakuwa na mambo mengi ikiwemo maonesho ya Mavazi, Dansi, Muziki kutoka kwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa jijini Mwanza.

Ameongeza kuwa watu watapata pia kuwajua watangazaji na historia ya radio hiyo tokea ilipoanza mpaka hapa ilipo, vile vile amesema kuwa kiingilio ni bure kwa watu wote na ulinzi utakuwepo wa kutosha kwa yeyote atakaefika hapo kesho katika viwanja hivyo.