advert

http://

Thursday 27 June 2013

MAHAKAMA YA WILAYA NJOMBE YAMFUNGA MAISHA MBAKAJI


.
Mahakama ya Wilaya ya Njombe juzi Imemuhukumu Kifungo Cha Maisha Jela Mkazi Mmoja wa Ramadhani Wilayani Njombe Kelvin Kigola Mwenye Umri wa Miaka 22 Baada ya Kupatikana na Hatia ya Kosa la Ubakaji.

Akisoma Hukumu Hiyo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe Agustino Rwezile Amesema Mahakama Imetoa Adhabu Hiyo Baada ya Kuridhishwa na Ushahidi Uliotolewa na Upande wa Mlalamikaji Mahakamani Hapo.
Amesema Mahakama Imemtia Hatiani Mtuhumiwa Chini ya Kifungu Kidogo  cha Sheria Namba 131 Sura ya 16 Kilichofanyiwa Marekebisho Mwaka 2002 na Kusema Adhabu Hiyo Inapaswa Kuwa Fundisho Kwa Watu Wengine Wenye Mwenendo Kama Huo.
Awali akisoma Mashtaka Mahakamani Hapo Mwendesha Mashtaka Atupakisie Mwakasitu Ameiambia Mahakama Kuwa Mnamo Sept 24 Mwaka 2012 Majira ya SaaSita Mchana Mtuhumiwa Alimbaka Binti Huyo Wakati Akitoka Kucheza.
Imedaiwa Mahakamani Hapo Kuwa Wakati Binti Huyo Anatoka Kucheza Alikutana na
Mshtakiwa Njiani Ndipo Alipo Mbeba na Kumpeleka Kichakani na Kumbaka na Kumtishia Kumchoma kisu Kama atamwambia  mtu yeyote.

Kwa Mara ya Kwanza Mtuhumiwa Huyo Alifikishwa Mahakamani Hapo Nov Mosi Mwaka 2012 na Kukana Kutenda Kosa Hilo.
Hii ni Mara ya Pili Katika Kipindi Kisichozidi Wiki Moja Kwa Mahakama ya Wilaya ya Njombe Kutoa Hukumu ya Kifungo Cha Maisha Jela Baada ya Kuwakuta na Hatia Watuhumiwa wa Makosa ya Ubakaji.

Wiki Iliopita Mahakama Hiyo Ilimuhukumu Kifungo Cha Maisha Jela Mkazi Mmoja wa Kijiji Cha Ikelu Baada ya Kupatikana na Hatia ya Kosa la Ubakaji.
Wakati Huo Huo Mahakama ya Wilaya ya Njombe Imemuachia Huru Mkazi Mmoja wa Mjimwema Makambako Esther Fute Mwenye Umri wa Miaka 28  Aliyekuwa Anakabiliwa  na Kosa la Kukutwa na Risasi 99 Nyumbani Kwake.

Hakimu wa Mahakama Hiyo Agustino Rwezile Amesema Mahakama Imeamuachia Huru
Mtuhumiwa Baada ya Upande wa Mashtaka Kushindwa Kuithibitishia Mahakama
Kama ni Kweli Mtuhumiwa Alikuwa Akimiliki Risasi Hizo.

NA GABRIEL KILAMLYA 

WANAWAKE wakiwezeshwa kiuchumi na ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu ya ujasiriamali, kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu haki zao katika jamii hali ya umaskini itapungua.

Kauli hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mfuko waFursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani.
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu,Benjamin Mkapa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii wajasiriamali hao kutoka mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani, ambapo jumla ya wanawake wapatao 264 wanashiriki.

“Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote umekusudia kwa nguvu zake zote kuendeleza vita ya hii ya kuwawezesha wanawake  nchini kujikwamua katika wimbi la umasikini, maradhi na ujinga,” alisisitiza Mama Mkapa.

Aidha ameiomba Serikali, asasi za kiraia, taasisi za dini na wahisani binfasi ndani na nje ya nchi, kusaidia wanawke haswa wa vijijini kujikwamua na umaskini. Mama Mkapa aliongeza kuwa mfuko huo,kwa kipindi cha miaka 16 zaidi ya wanawake 6,820 wamepata mafunzo ya stadi za biashara na wengine 4,500 wamepata fursa ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kupitia EOTF ili kutangaza na kuuza bidhaa zao.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah Kigoda akifungua mafunzo hayo alisema Serikali imeanzisha utaratibu wa kuweka kumbukumbu za mkopo katika mabenki kwa kupitia ‘Credit Reference Bureau’ ili kuweza kusaidia kuwafahamu wateja, na kuwaasa wajasiriamaliwanapokopa wakumbuke kulipa kwani uaminifu ni kitu muhimu katika biashara.

“Suala lingine la kulipa kipaumbele ni lile la kuongeza thamani ya mazao wanayoyazalisha na tuache kuwazalishia watu wengine bidhaa wakaenda  kuongezea thamani kidogo tu kama vile kwa kufunga na kuweka
nembo ya kibiashara na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Dk. Kigoda.

Aliahidi kuwa Wizara yake iko makini kufanya linalowezekana kushirikiana na wajasiliamali hao kutatua tatizo hilo la kuuza malighafi badala ya bidhaa iliyoongezwa thamani ili kuongeza ajira na kupunguza
umaskini.

Edwin Moshi

MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Pamojana ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.


Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa lasita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

“Siyo siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majiraniwanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitakelazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi
ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua
jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.
“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe
mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako
anamfulia nguo. 
Edwin Moshi.

Kiukweki kamponda sana Prezzo na pia hata mademu wake,kasema hajui muziki zaidi ya kutafuta wasichana.Amesema hapa Bongo yuko na mtangazaji wa radio ambaye hachoki kumfagilia Prezzo.
Kadai Kenya ndo balaa tupu mpka mke wake kamtwanga talaka.
Kaenda mbali zaidi na kudai kwamba Prezzo hajui muziki na hata show zake za nje bei yake ni sawa na bure na kule anafuata wanawake sio kazi yake ya muziki.
Huyu dada ambaye ni Mkenya na pia promoter wa wasanii Ulaya,Ujerumani na nchi kibao za huko,
Amemfagilia sana Jagur na kudai anaweza na show zake Ulaya ziko juu kwa bei na kila kitu.

Ashley Toto katika akaunti yake ya facebook, amendika hivi :
Sijui kuna beef gani hapo.....mmhh 


KINYANG’ANYIRO cha kumpata Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu kinazidi kushika kasi na sasa, kazi kubwa ipo katika ngazi ya kanda, pale kutakapokuwa na kazi ya kumsaka mrembo wao ndani ya wiki hii.
Kazi kubwa itakuwa katika kumpata Redd’s Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Redd’s Miss Kanda ya Mashariki na Redd’s Miss Kanda ya Ziwa.
Shughuli itaanza kesho, wakati warembo zaidi ya kumi watakapopanda jukwaani katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtende, uliopo Soweto Mbeya, kumsaka Redd’s Miss Nyanda za Juu Kusini.

Katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza saa 2 usiku, burudani kali inatarajiwa kutolewa na bendi ya FM Academia, huku kiingilio kikiwa ni Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 25,000 kwa viti maalumu.

Keshokutwa itakuwa kazi pevu kwa warembo wa Redd’s Miss Kanda ya Mashariki, ambao watapanda jukwaani katika hoteli ya Nashera mjini Morogoro, kumsaka yule atakayefanikiwa kutwaa taji.
Wanne Star pamoja na wasanii wengine wa Morogoro ndio watakaonogesha shindano hilo, ambalo kiingilio chake kitakuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 20,000 viti maalumu.

Siku hiyo pia atasakwa Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, shindano ambalo litafanyika katika ukumbi wa Nyerere ndani ya hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

Pia kutakuwa na burudani za kumwaga zitakazoongozwa na mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akishirikiana na Michael Ross na kiingilio kitakuwa Sh 20,000 viti vya kawaida na Sh 40,000 viti maalumu.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Michuzi
Jamaa anaitwa Salu B.Ni msanii wa bongo flavour na pia ni Producer mzuri sana pale Imotion records kiwalani DSM akishirikiana na Bwana Kisaka.

Mar nyingi Wasanii wanawachezea wadada zetu ila yeye kaamua kufanya kweli na hapo jana mpenzi wake alijifungua mtoto wa kiume.Bado Bwana Kisaka.
Ikumbukwe imotion records imewatoa wasanii wengi kama Sam wa Ukweli,Best Nasso,Uncle G na wengine kibao.Babamzazi.com inawapa pongezi 
kwa kuinua vipaji vya wasanii hapa Tanzania.

KULITOKEA kisa hiki ni katika eneo la Baharini  katika eneo la Eldoret Magharibi pale mwenye boma alipoamka na kumpata mbwa wake akila kichwa cha binadamu.
Bw Julius Kemboi alisema mbwa huyo alikuwa mlangoni mwake huku akila  kichwa hicho ambacho kilikuwa kimeanza kuoza.

Bw Kemboi aliongezea kuwa alikimbia katika kituo cha polisi kilicho karibu naye cha Baharini kuripoti tukio hilo na aliporudi na mafisa wa polisi kuona tukio hilo, kichwa hicho kilikuwa hakipo tena.

“Niliamua kwenda kuwaarifu polisi na tuliporudi nao ili wakichukue, hatukikipata
tena na sielewi kilikuwa kimeenda wapi,” alisema Bw Kemboi.

Alisema kuwa haelewi ikiwa kichwa hicho kilichukuliwa na mbwa tena hadi mahali
pengine walianza msako katika kichaka kilicho karibu na ambapo waliupata
mwili bila kichwa huku ukiwa umeliwa na mbwa sehemu kadha.

Mafisa hao wa polisi waliuchukua mwili huo na kuupeleka katika hifadhi ya maiti ya
hospitali kuu ya rufaa na mafunzo ya Moi mjini Eldoret.
Naibu wa afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Charles Mutua alisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Mwili huo ulikuwa wa mwanamme.
Posted: 26 Jun 2013 04:59 AM PDT


Toka pande za Arusha jamaa anaitwa Stopa.Ni msanii mkongwe kwenye game.Kwa sasa amekuja na wimbo wake mpya akiwa na Joh Makini anakwambia ameshavurugwa.Isikilize na kuipakua ukiipenda.



Kiongozi wa Terror Squared Joseph Antonio Cartagena a.k.aFat Joe Clack the Don ana kila sababu ya kuufatisha wimbo wa Snura ‘Majanga’kimyakimya, duh..Bahati mbaya ni Kiswahili and he speaks English only!

Wiki hii ilianza vibaya kwa rapper huyu ambapo siku yajumatatu mahakama ya Newark ilimhukumu kwenda jela miezi 4 na kulipa faini ya kiasi cha $15,000, baada ya kushindwa kulipa kodi kutokana na kiasi cha zaidiya  $3.3 million alizoingiza.
Ripoti zinasema mwezi December Fat Joe alinusurika kwenda
jela baada ya kushindwa kulipa kodi ya kipato cha zaidi ya $ 1million
alichoingiza kwa mwaka 2007-2008 na kuahidi kulipa kiasi hicho, ombi ambalo
lilikubaliwa na mahakama.
Lakini Fat Joe hakufanya hivyo na kujikuta kalimbikiza deni
ambalo limemshinda kulipa, rapper huyo alikiri mashtaka na kuiomba radhi
familia yake na watu wote wanaomsapoti.
Anatakiwa kuripoti gerezani August 26 au kabla.
Posted: 26 Jun 2013 12:40 AM PDT

MASHIRIKA yanayoshughulikia haki za albino nchini
Kenya yamewataka watu wanaoishi na hali hiyo kususia shughuli ya kuwahesabu
kwa madai kuwa  maandalizi ya zoezi hilo yalifanywa kiholela bila wao
kushirikishwa.


Mashirika ambayo yanajumuhisha Chama cha Maalbino nchini (ASK) na Mtandao wa kuwawezesha  Maalbino 
(AEN), yalishutumu Baraza kuu la kitaifa la Kushughulikia Watu Wanaoishi
na Ulemavu (NCPWD) kwa kuendesha sensa kabla ya kufanya uhamasisho wa
kutosha kupitia vyombo vya habari ili kuwaandaa walengwa huku wakidai
hiyo ilikuwa njama ya baadhi ya watu katika baraza hilo kufuja fedha
zilizotengewa maalbino.

“NCPWD haiwezi kuendesha zezi la
kuwahesabu watu wanaoishi na ulemavu bila kuwashirikisha washikadau
ambao wanafanya kazi kwa karibu na walengwa wala kuwahamasisha kupitia
vyombo vya habari.
Hiyo ni njama ya baadhi ya viongozi ndani ya NCPWD 
ambao wanapinga kuwekwa kwa hazina ya watu wenye Ulemavu wa ngozi,” 
akasema Bw Mwaura Maigua Isaac, ambaye pia ni mkurugenzi wa kitaifa wa
Chama cha watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi nchini (ASK) na mbunge wa
kuteuliwa kupitia Chama cha Orange Democratic movement (ODM).
Akaongezea, “ Kwa hiyo tunawataka
wanachama wetu wasijitokeze kwa ajili ya zoezi hilo tatanishi. Vilevile,
tunaitaka serikali kusimamisha shughuli hiyo hadi hatua mwafaka
zifuatwe la sivyo zoezi hilo halitafua dafu.”

Aidha, mashirika hayo yalishutumu
vigezo vilivyotumika katika utoaji wa kandarasi ya uagizaji wa mafuta ya
losheni ya kuzuia jua kutoka nchi za nje ambapo chupa moja ya losheni
hiyo inagharimu sh 1,500 ilhali chupa ya aina hiyo inauzwa sh700 humo
nchini.
“Tunataka kuionya serikali kuwa
huenda ikapoteza jumla ya sh22 milioni na hivyo kuna haja ya serikali
kuanzisha uchunguzi ili kunusuru nchi kupoteza kiasi hicho kikubwa cha
fedha ndani ya mifuko ya watu,” akasema Bw Isaac.
Mashirika hayo pia yalilitaka bunge
la kitaifa kubuni kifungu cha sheria ambacho kitasaidia kuwalinda watu
wanaoishi na ulemavu wa ngozi.
Zoezi la kuwahesabu watu wenye ulemavu wa ngozi lilianza mnamo Juni 24 
na linatarajiwa kumalizika July 5.
Na LEONARD ONYANGO
Posted: 25 Jun 2013 11:58 PM PDT
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.
Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 30 za kimarekani hadi dola Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.
Posted: 25 Jun 2013 11:48 PM PDT
Posted: 25 Jun 2013 11:26 PM PDT
Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam jana mchana.
Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki.

Source:udakuspecially
Kwa nn hawa dada zetu ukianza nao uhusiano uwa wanamgeuza mwanaume ndo kila kitu yan ndo kama wazaz wake mana atataka umlishe,umnunulie vitu kama nguo za ndan na umlipie ada,how come majukumu ya wazaz wako yawe yangu?ina maana mimi sina ndg wa kuwajal mpaka nikuangaikie wewe.
Mnaboa sana masista due njaa mana mtu akikuambia hana kitu unamchukia na akikuambia kwan mwanzon kabla hujawa na mm ilikuaje?anasema usinione kama nna dhiki sana ila kwa hali ilivo ni kama una dhiki
Mnafanya wanaume tusione thaman ya hela yetu na tuone thaman ya kukupendezesha wewe wakat tuna ndugu na jamaa wana shida na tuna wajibu wa kuwasaidia.
Samahan kama nimekukwaza ila nimeongea uhalisia na vitu ambavyo vmentokea na imeniuma sana mana mdada anasema simpend kwa sabab nimeshndwa kumtimizia mahitaj yake na nimemjibu kama mapenz ni hayo then mimi sipo tayari na huko huru kufanya uamuz unaotaka na analaum kua nimemuharibia maisha.

Source:Jamii forums
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa,  amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta.
Tendwa  ameyasema   hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp  kuhusu  hatua  zitakazochukuliwa...
Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu.
Source :Jamiiforum


Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo. 



Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.


Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.


Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.

Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.


Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.


Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria. 


Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashi Mohammed aliomba mwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.

“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisema Silima.


Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.


Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na Tanzania Law Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake na kuanza kumshambulia.”


Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi, ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.
“Kwa msingi huo, tarehe 28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali Na 290, nilitumia maneno ‘mauaji yanayofanywa kisheria’ nikimaanisha mauaji yanayotokea katika mazingira niliyoeleza..,”alisema Silima.

Hata hivyo alisema siyo nia ya Serikali kuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyo vinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu.

Alibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kuheshimu haki za raia na kutumia busara kutatua migogoro.

Hata hivyo, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imelaani kauli ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi iliyoitoa jana na kueleza kuwa haikubaliani nayo kwa kuwa inatoa baraka kwa polisi kuendeleza mauaji ya raia.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kikao cha bunge kuahirishwa, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa kambi hiyo rasmi, Vicent Nyerere alisema kauli hiyo ingekuwa na uthabiti kama askari polisi wangekuwa waadilifu.


“Kauli ingekuwa thabiti kama polisi wangekuwa waadilifu. kabla ya kutoa kauli hiyo, Serikali ilitakiwa kuchuja miongoni mwa askari wa jeshi la polisi, wa ngazi zote na kuwaondoa wasio waaadilifu ndipo wakatoa kauli hiyo wananchi wataielewa Serikali,”alisema Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini(Chadema).


Kwa upande wake, Mbunge wa Ole, (CUF) Rajab Mbarouk Mohammed akizungumzia kauli hiyo ya Serikali alisema kuwa majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima ni ya kisiasa.


Alisema kwamba kauli hiyo ni mwendelezo wa kauli iliyotolewa Alhamisi iliyopita na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwataka pilisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote watakaokaidi kutii sheria.


“Hakuna mwenye haki ya kuua, kuua ni kuua tu. Mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kifo baada ya kumtia hatiani mshtakiwa husika. Lakini kuwa polisi wanafundishwa utii, siyo kuua,”alisema Rajab.

Alifafanua kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na kwamba kuruhusiwa kujihami haimaanishi kuua raia.
Nao Wabunge Aeshi Hilaly na Aly Keissy walisema ni vizuri raia wakatii mamlaka iliyopo na kutekeleza utii wa sheria bila shuruti.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu alisema: “Maoni yangu haki za watuhumiwa lazima ziheshimiwe.”
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS), Francis Stola alisema hakuna sheria inayompa mamlaka askari polisi kutumia nguvu za ziada ikiwemo kupiga raia pindi anapotekeleza majukumu yake,isipokuwa tu anaweza kutumia nguvu kiasi iwapo raia anayekabiliana naye anaonyesha vitendo vya kukaidi amri ama kuhatarisha usalama.


Stola ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kauli bungeni alisema kuwa kwa kufuata sheria polisi haruhusiwi kupiga raia. “ Ukisoma sheria hakuna mahala utakuta kuna neno limeandika piga…. Askari polisi anachoweza kufanya ni arrest(kamata) na siyo vinginevyo, hana mamlaka kabisa ya kupiga raia”

Alisema sheria imetamka wazi kuwa kunapojitokeza hali yoyote inayopaswa kdhibitiwa na vikosi vya ulinzi, nguvu inayopaswa kutumika ni ile ya kawaida na kwamba kitendo cha kutumia risasi za moto ama kupiga raia ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

Alisema polisi anapaswa kutoa mwongozo kwa raia kumwelekeza jambo la kufanya iwapo kunajitokeza hali ya sintofahamu,lakini hapaswi kutumia nguvu kupita kiasi ikiwemo kuwapiga raia

“ Sheria inasema wazi kwamba panapojitokeza hali yoyote korofi, polisi wanatakiwa kutumia nguvu ya kawaida tu kukabiliana na hali hiyo na wala siyo kutumia silaha za moto… silaha za moto zinaweza kutumika tu iwapo kunajitokeza tukio ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa maisha ama mali isipotee” alisema

Kuhusu wananchi kufanya maandamano, rais huyo alisema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia,lakini yanafanyika katika utaratibu maalumu. “ maandamano ni haki ya kila raia lakini panapaswa kuwa na utaratibu maalumu…. Kama kunajitokeza maandamano ambayo hayana utaratibu polisi wanapaswa kutumia reasonable force (nguvu ya kawaida) kudhibiti maandamano hayo na wala siyo kutumia nguvu za ziada.

 Mwananchi:
Posted: 25 Jun 2013 11:07 PM PDT

Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.

Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.


Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.


Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.

“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.

Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.

“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.


Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.


Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).


Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.

“Ulinzi ni mkali mno, yapo masharti kadhaa wanayoyataja kuwa yatatumika kwa watu watakaoingia eneo la uwanja au kuisogelea ndege ya Rais Obama. Jamaa wameweka masharti magumu,” alisema.


Mkurugenzi huyo alisema maofisa hao wanakuja kwa makundi na hivi karibuni lilifika kundi la kusimamia mawasiliano ambayo yatatumiwa wakati watakapokuwa nchini.

“Pia wamechukua kwa muda karakana ya Shirika la Ndege la Precision Air iliyoko kwenye eneo la Uwanja wa Ndege. Maofisa wa Usalama wa Marekani wanataka kufanya shughuli ndani mle,” alisema Malaki.

Pia, ndege mbovu zilizokuwa kwenye maeneo ya uwanja huo zimeondolewa. Viongozi wa Precision Air hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili Manongi alisema ni utaratibu wa kawaida kwa karakana kuazimwa wakati wanapokuja wageni mashuhuri.

“Nafasi ile mara nyingi hutumiwa na maofisa wa usalama pale wanapokuja wageni mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,” alisema.


Alidokeza pia pamoja na ugeni wa Rais Obama, pia kumekuwa kuna presha ya ugeni wa marais wa nchi mbalimbali duniani wanaokuja kuhudhuria mkutano wa Smart Partnership unaonza keshokutwa.

Pia wana kazi ya kuwapokea wake za marais wa Afrika watakaokutana na mke wa Rais Obama, Michelle na mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, George Bush, Laura.
Kazi inayofanyika

Ofisa mmoja wa Uwanja Ndege ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema maofisa hao walifanya ukaguzi wa hali ya juu kwenye sehemu mbalimbali za uwanja huo wakitumia mitambo maalumu ya kung’amua mabomu.

“Hawa jamaa wako juu sana katika mambo ya usalama maana wana kifaa cha kuchunguza mabomu hata yaliyo chini ya ardhi,” alisema na kuongeza kuwa licha ya kukagua uwanja huo, pia walikwenda mbali zaidi na kukagua maeneo ya jirani.

Mitambo mbalimbali ya shughuli za usalama imefungwa kwenye eneo hilo la uwanja na maofisa wa Marekani walionekana wakiwa juu ya paa la moja ya majengo ya uwanja huo wakifunga mitambo katika minara mirefu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano.

Yavuruga ratiba za ndege
Manongi alisema kampuni za ndege zimeagizwa kufanya mabadiliko ya ratiba za safari siku atakapowasili Rais Obama ili kutoa nafasi kwa anga hilo kutumika kwa shughuli za mapokezi yake.

Alisema kampuni zote za ndege zimeshapewa taarifa kuhusu hatua hiyo.

“Kubadilishwa kwa ratiba kunatokea mara kwa mara na huwa tunawapa taarifa kampuni za ndege mapema ili wajue namna ya kujipanga,” alisema Manongi.

Kutua Senegal leo
Rais Obama anatarajiwa kuanza ziara yake ya barani Afrika leo na alitarajiwa kutua Dakar, Senegal saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.

Akiwa nchini humo, ratiba inaonyesha kuwa atakuwa na mazungumzo na Rais wa Senegal, Macky Sall kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Pia ratiba hiyo inaonyesha kuwa atakutana na majaji kutoka mikoa yote ya nchi hiyo.

Pia atakwenda katika Kisiwa cha Goree ambacho kiko kwenye Bahari ya Atlantic na atatembelea Jumba la Makumbusho katika kisiwa hicho ambacho kilikuwa kituo cha kuhifadhi watumwa waliokuwa wanasafirishwa kutoka Afrika kwenda Marekani.

“Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa kabla ya kupumzika kwa muda mfupi na kuanza safari ya kwenda Afrika Kusini,” ilisema taarifa hiyo ya Ikulu ya Marekani.

Mwananchi:
Posted: 25 Jun 2013 11:04 PM PDT

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi wa madiwani kata nne za Arusha hadi Julai 14 kuruhusu kurejea utulivu baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema ulioathiri uchaguzi huo wiki iliyopita.


Bomu hilo lilirushwa Juni 15 na mtu asiyejulikana katikati ya mkutano wa Chadema katika viwanja vya Soweto, mjini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa na uchaguzi huo wa Juni 16 kulazimika kuahirishwa.


Baada ya tukio hilo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Arusha aliuahirisha hadi Juni 30, lakini jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema utafanyika Julai.

Kata zinazohusika ni Elerai, Kimandolu, Thani na Kaloleni. Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Lubuva alisema walipotangaza kuwa uchaguzi ungefanyika Juni 30 waliamini kuwa hali ya utulivu na amani ingekuwa imetengemaa.

“Lakini kwa bahati mbaya tumejiridhisha kuwa hali bado inahitaji kuangaliwa kuhakikisha imerejea katika utulivu wake kikamilifu. “Hiyo haimaanishi kuwa ni mbaya, isipokuwa tumeona bado tunahitaji muda wa kama wiki mbili hivi kuona vumbi lililokuwa likitimka limetulia,” Jaji Lubuva alisema.

Kwa mujibu wa Jaji Lubuva, wapiga kura hawapaswi kutekeleza haki yao ya kupiga kura katika wasiwasi hivyo ni wajibu wa Tume kuhakikisha unaondoka na wapiga kura wanatekeleza haki yao kwa amani.


“Tunataka watu wajihisi huru wakati wa kupiga kura, ndiyo maana tumeahirisha uchaguzi wa kata hizo kwa mara nyingine. Wanapokuwa na amani na uhuru wapiga kura wanaweza kuchagua wanayemtaka kwa utaratibu mzuri, vinginevyo, shughuli yote ya kupiga kura inaweza kuharibika,” alisema Lubuva.


Aidha, alitaka wagombea na vyama kutoendeleza kampeni kwa sababu kuahirishwa kwa uchaguzi hakumaanishi kuwaongeza muda wa kujinadi au kutafuta wapiga kura wa kuwaunga mkono.

“Muda wa kupiga kura haujabadilika. Vituo vya kupigia kura havijabadilika na vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. 


Waliokuwa katika mstari ndio watakaopiga kura na watakaofika vituoni baada ya muda huo kwisha hawataruhusiwa kupiga kura ili kutoa nafasi ya kura kuhesabiwa,” alisema.


Jaji Lubuva alisema matokeo ya uchaguzi huo mdogo yatatangazwa mapema na taratibu za uchaguzi zitazingatiwa ili kutoa haki kwa wapiga kura na wanaopigiwa kura.


Inadaiwa bomu hilo lililokuwa kwenye mfuko wa plastiki, lilirushwa na mtu asiyejulikana. Waliopoteza maisha katika tukio hilo ni Amir Ally (7), Judith Moshi na Amir Ally.

Habari Leo: