advert

http://

Wednesday, 9 October 2013

MAAJABU YA MTOTO ALIYEFUFUKA MENGI YAJITOKEZA BAADA YA KABURI KUFUFULIWA

.

Stori:Victor Bariety, Geita 
TUKIO la mtoto Shaaban Maulid, 16, aliyefariki dunia miaka mwili iliyopita kabla ya mwaka huu kuonekana (kufufuka), limeendelea kutikisa baada ya maajabu mengine kujiri.


Shaaban, alifariki dunia na kuzikwa Januari, 2011 lakini Septemba 30, mwaka huu, alionekana akiwa hai, ingawa alikuwa akizungumza kwa taabu.
Kwa vile kufufuka kwa Shaaban ni jambo lililoacha wazi midomo ya wengi hususan waliohudhuria mazishi yake miaka miwili iliyopita, ilibidi kaburi alilozikwa lifukuliwe ili ndani yake ijulikane kuna nini.
Tamko la kufukua kaburi la Shaaban ni azimio la kifamilia, hasa baada ya ndugu na majirani kupendekeza, kwani kufufuka kwake, kulivuruga vichwa vingi, wapo walioamini inawezekana, ila wengine wakipinga kwamba mtoto huyo aliyeibuka sasa ni mzimu tu.

MAUZAUZA KABURINI
Shaaban alizikwa kwenye eneo la nyumba ya baba yake, Maulid Shaaban, kwa hiyo haikuwa shida kulipata kaburi, kwani familia nzima na hata majirani wanalijua kwa sababu walishiriki kumzika.
Jumatano iliyopita, shughuli ya kufukua kaburi la Shaaban ilifanyika. Kazi hiyo ilianza saa 2 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, kabla ya kukamilika saa 4.30 asubuhi.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa kipindi chote ambacho ufukuaji ulifanyika, mauzauza mengi yalitokea, hivyo kusababisha taharuki na hata watu wengine kutimua mbio.
Wakati shughuli ya ufukuaji ikiwa mbichi kabisa, alitokea mbwa kutoka kusikojulikana ambaye alifika na kuanza  kujigalagaza juu ya kaburi hilo, huku akibweka. 
Hali hiyo, ilitafsiriwa na wengi kwamba mbwa huyo alikuwa hataki kaburi hilo lifukuliwe, ingawa baadaye aliondoka taratibu akibweka na kutokomea kusikojulikana.
Saa 2.30 asubuhi wakati ufukuaji ukiendelea, mwanamke jirani anayeitwa Sharifa Hitler, alianguka na kupoteza fahamu, kabla ya kuzinduka dakika 20 baadaye, kufuatia jitihada za kumuwekea kipande cha sabuni mkononi.
Baada ya kuzinduka, Sharifa alisema kuwa alisikia kichwa kinakuwa kizito, akapatwa na kizunguzungu kisha akapoteza fahamu.
Saa 3.05 asubuhi, tukio lingine litokea, kwani kipindi kaburi linafukuliwa, ukuta wa nyumba ya baba yake Shaaban, nao ulianguka na kutoa sauti yenye mshindo mkubwa.
Sauti hiyo iliwatisha wengi, kwa hiyo watu walikimbia kwa kutawanyika, kila mmoja akishika uelekeo wake.
Kuanguka kwa ukuta huo, kulifanya kazi ya kufukua kaburi isitishwe kwa muda ili kutawanya kifusi cha ukuta wa nyumba, kuhakiki kama kuna mtu aliangukiwa na kufunikwa.
Hata hivyo, baadaye iliamriwa mambo yote mawili yafanyike kwa wakati mmoja, baadhi wahusike na utawanyaji wa kifusi na wengine waendelee kufukua kaburi ili kwenda na muda.

MAAJABU NDANI YA KABURI
Kule kwenye kifusi, ilionekana hakukuwa na tatizo lolote lakini kwenye kaburi baada ya ufukuaji kukamilika, mambo yaliyoonekana ni haya;
Mosi; kwa mila za Kiislam, ndani ya kaburi, kuna sehemu ndogo ambayo huchimbwa kulingana na kimo cha marehemu, kisha kulazwa ndani yake.
Sehemu hiyo huitwa mwanandani, kwa hiyo baada ya kufukua, badala ya kukuta mwili, wafukuaji walikutana na chungu kikubwa.
Pili; kile chungu kilikuwa kimefunikwa na mifuko aina ya viroba. Tafsiri ya wengi walioshuhudia tukio hilo ni kwamba sanda aliyozikwa nayo Shaaban miaka miwili iliyopita, ndiyo iliyogeuka kiroba.
Tatu; ndani ya chungu kulikuwa na mifupa ya kiumbe cha ajabu, kwani kwa muonekano haifanani na ya binadamu wala mnyama yeyote anayefahamika, kwani ilikuwa ni midogomidogo mno.
Nne; kulikuwa na madawa yenye umbo la kimimika, rangi nyeusi.
Dunia Mrisho ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo na alikuwepo miaka miwili iliyopita wakati Shaaban akizikwa, alisema kuwa yaliyoonekana ndani ya kaburi hilo, yamewashangaza wengi.
“Huyu mtoto tulimzika kwa heshima zote za Kiislam na mwili wake ulikuwa kwenye sanda, hii mifuko ndani ya kaburi imetoka wapi? Tunashangaa pia kukuta chungu ndani ya kaburi na kina mifupa na yule mbwa aliyetokea na kutokomea ni wa nani? Hapa kuna kitu,” alisema Dunia ambaye ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

KWANI SHAABAN ALIKUFAJE?
Januari Mosi, 2011, Shaaban akiwa na afya njema kabisa, aliondoka nyumbani kwao asubuhi kwenda kuchunga mbuzi kwenye malisho.
Tangu siku hiyo, Shaaban hakuonekana tena, ingawa jitihada za kumtafuta zilifanyika kwa nguvu sana kwa usimamizi wa jeshi la polisi.
Katika eneo la malisho, mbuzi alioondoka nao Shaaban walionekana wakiwa katika idadi kamili lakini mtoto huyo ndiye hakuonekana.
Siku nne baadaye, Shaaban alikutwa akiwa amefariki dunia na mwili wake ulikutwa ndani ya kisima katika Mtaa wa Mbugani, Geita.
Baada ya kujiridhisha kwamba amefariki dunia na wazazi wake kumtambua kwamba ni mtoto wao, alizikwa katika makaburi ya eneo la nyumbani kwao.

SHAABAN ALIFUFUKAJE?
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mama mzazi wa mtoto huyo, Aziza Ramadhani, 45, ambaye alisimulia jinsi alivyoweza kumuona mtoto wake huyo akiwa hai.
“Ilikuwa Septemba 30, mwaka huu, nilikuwa naelekea sokoni kwenye shughuli zangu za kuuza mbogamboga. Ilikuwa saa 1.30 asubuhi, nikiwa Mtaa wa Nyankumbu, nilikutana na mwanangu Shaaban.
“Nilishtuka na sikuamini haraka. Nilimwita kwa jina lake, mwanangu Shaaban ni wewe? Akaniitikia kwa kutikisa kichwa. Hakuweza kutoa sauti vizuri, alikuwa anazungumza kwa taabu.
“Nilikwenda kumshika mkono kuhakikisha kuwa ni binadamu au mzimu huku nikiwa siamini kabisa kuwa ni yeye. Nilipoona kuwa ni yeye nilimpigia simu mume wangu, akaja tukamchunguza vizuri na kubaini kuwa kweli ni mtoto wetu Shaaban.
“Ni maajabu kabisa, sisi tuliamini amekufa na tukamzika miaka miwili iliyopita. Kweli hii dunia ni ya maajabu,” alisema Aziza ‘Mama Shaaban’.
Aliendelea kusema kuwa mtoto huyo alikuwa na alama ya kinundu kwenye paji la uso na mguuni ambalo ni kovu iliyosababishwa na kuchomwa na mwiba. 
Aliongeza kuwa vilevile Shaaban alikuwa na mwanya uliofanana na wa baba yake ambapo huyu alama zote hizo anazo.
Alisema kuwa walikagua alama hizo kipindi cha kuutambua mwili wake pale alipofariki dunia na kujiridhisha ndipo walipomzika.
“Baba yake alipokuja eneo la tukio, tulimpeleka hospitali kwa sababu hali yake haikuwa nzuri, mpaka sasa bado yupo hospitali akitibiwa,” alisema Aziza.

SHULENI KWAKE NAKO
Mtoto huyo aliyevuta hisia za watu wengi mjini Geita, amethibitishwa na walimu wake katika shule aliyokuwa anasoma kwamba ndiye aliyezikwa.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwatulole, Geita, Joseph Nungula, alisema kuwa amemwangalia Shaaban na kujiridhisha ni mwanafunzi wake yuleyule ambaye miaka miwili iliyopita zilitolewa taarifa za kifo chake na baadaye kuzikwa.
“Nimemtambua mtoto huyo kwa sura na alama, hasa ya usoni na alikuwa na mahudhurio mazuri shuleni. Pia maendeleo yake kitaaluma yalikuwa mazuri,” alisema mwalimu huyo huku akiungwa mkono na wanafunzi waliokuwa wanasoma na Shaaban.

BABA ANAZUNGUMZA
Maulid Shaaban ‘Baba Shaaban’, alisema kuwa ni kweli kabisa mtoto wao alitoweka na alipatikana akiwa ameshafariki dunia.
Aliongeza, mwili wa Shaaban ulikutwa ndani ya kisima cha maji, hivyo walitoa taarifa polisi kisha waliruhusiwa kuchukua mwili.
“Daktari alithibitisha alimkagua na kujiridhisha kwamba ameshakufa. Tukaamua kumzika kwenye kiwanja cha nyumbani kwangu, Kitongoji cha 14, Kambarage, hapa Geita.
“Shughuli zote za matanga tulifanya, baada ya hapo hatukuwa na wazo la Shaaban kurudi duniani. Leo hii kila kitu tunaona ni maajabu, Shaaban huyuhuyu ambaye tulimzika amerudi duniani,” alisema Maulid.

DAKTARI AELEZA
Shaaban amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, akifanyiwa uchunguzi zaidi na matibabu zaidi kwa sababu bado hajaweza kuzungumza vizuri.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Geita, Dk. Adamu Sijaona anayemtibu mtoto huyo, alisema kuwa tayari wazazi wake wameshachukuliwa sampuli na kuhifadhiwa kwenye maabara na mifupa iliyokutwa kaburini imechukuliwa kwa uchunguzi wa DNA.
“Hali yake inaendelea vizuri hasa katika kutamka maneno ikilinganishwa na wakati anafikishwa hospitalini kwa mara ya kwanza kwa sababu alikuwa hawezi kutamka neno hata moja,” alisema Dk. Sijaona.

OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Mchunguzi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Ziwa, Lukas Nduguru, aliliambia gazeti hili kuwa wamechukua vipimo vya wazazi na mtoto pamoja na baadhi ya mabaki ya mifupa iliyokuwa kwenye kaburi hilo kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini mwili wa nani ulizikwa kwenye kaburi hilo.
“Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ilipata taarifa za huyo mtoto aliyezikwa mwaka 2011 kwamba ameonekana akiwa hai, kwa hiyo majibu ya vinasaba yatatoka ndani ya siku 14 au mwezi mmoja.
“Tuna changamoto za kukatika umeme mara kwa mara, kwa hiyo ndani ya kipindi hicho tutakuwa tumekamilisha,” alisema Dk. Ndunguru.

NENO LA KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo, mbali na kuthibitisha kufukuliwa kwa kaburi hilo kwa kibali maalumu cha mahakama, alisema mtu hawezi kufa kisha kufufuka kwa hiyo jeshi la polisi haliamini kama mtoto aliyezikwa ni yeye.
“Unajua hatuna imani na hili isipokuwa tunasubiri majibu ya uchunguzi wa watalaamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali,” alisema Paulo.

NI TUKIO LA PILI GEITA
Tukio kama hilo ni la pili kutokea katika Wilaya ya Geita katika kipindi kisichozidi miezi mitano ambapo Aprili 12, mwaka huu, mwanamke aliyetambulika kwa jina la Flora Onesmo, 45, aliyefariki dunia Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kisha kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, alionekana akiwa hai.
Flora, alikutwa hai Aprili 12, mwaka huu, akiwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kijiji cha Kasamwa, Geita.

UWAZI LIPO KAZINI

Uwazi bado lina kazi ya kufanya kuhusiana na Shaaban na Flora, yapo maswali mengi hayajajibiwa, kwa hiyo lipo kazini likiibuka litakuwa na mengine mengi ambayo pengine yatakuwa mazito zaidi. MHARIRI


Source:Global publishers

Stori: Makongoro Oging’
AHADI ya Mchungaji Anthony Lusekelo au Mzee wa Upako katika msiba wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God  Tanzania (EAGT) Dk. Moses Kulola ya rambirambi ya shilingi milioni 15 imezua utata baada ya kiongozi huyo kutoitimiza.


Ahadi hiyo alitolewa na Mzee wa Upako siku ya kuuaga mwili wa kiongozi huyo Agosti 31, mwaka huu katika kiwanja cha Kanisa la EAGT, Temeke ambapo viongozi kadhaa wa makanisa akiwemo  Mchungaji Lusekelo walitoa ahadi zao za rambirambi.


Hata hivyo, utata unakuja kwani Mzee wa Upako mpaka Jumapili iliyopita fedha zake zilikuwa hazijafika kwa kamati husika inayoratibu rambirambi hizo.


Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba wachungaji na maaskofu walioahidi wameshatimiza ahadi zao ndani ya siku nne baada ya kuuaga mwili lakini kwa upande wa Mzee wa Upako bado hajatimiza ahadi yake.


Mzee wa Upako ndiye mchungaji pekee aliyewashinda wenzake kwa kutangaza dau kubwa la rambirambi kiasi cha shilingi 15,000,000.


Askofu Kulola alifariki dunia  Agosti 29, mwaka huu ambapo sasa ni zaidi ya mwezi mmoja na siku kadhaa.


 Mweka Hazina wa Kanisa la EAGT kanda ya Dar es Salaam, Mchungaji Praygod Zawadi Mgonja ndiye aliteuliwa na uongozi wa kanisa hilo kuratibu, kupokea rambirambi na ndiye alikuwa akisimamia matumizi.


Gazeti hili liliwasiliana kwa njia ya simu ya kiganjani na Mchungaji Mgonja na kumuuliza kama ameshapokea mchango huo toka kwa mtumishi huyo wa Mungu ambapo alisema kwamba hajapokea na kudai kwamba huenda ameshapeleka mwenyewe kwa familia ya marehemu.


“Pamoja na kwamba ahadi hiyo kutonifikia huenda aliamua kupeleka kwa wana familia, jaribu kuwasiliana nao,”alisema Mchungaji Mgonja.


Mwandishi alimtafuta mtoto wa marehemu aitwaye Willy Kulola na alipoulizwa kama amepokea mchango wa rambirambi kutoka kwa Mzee wa Upako alisema familia haijapokea fedha hizo.
“Hatujapokea labda mumuulize Mchungaji Mgonja kwani ndiye aliteuliwa kuratibu mambo hayo,” alisema.
Mzee wa Upako alipoulizwa alikiri kuwa fedha hizo hajaziwasilisha kwa wahusika kwa madai kwamba hapendi kumpa Mchungaji Mgonja wala mtoto wa marehemu bali anataka kumkabidhi mke wa Askofu Kulola.
“Napenda taarifa hizi zimfikie 
mke wa Mzee Kulola ili anifuate na nitampa rambirambi hiyo hata kama ni kesho akija nitamuandikia cheki,” alisema.
Alipoulizwa endapo anaweza kutoa fedha hizo kwa mtoto wa marehemu, alisema hawezi kumpa labda kama atakuwa amemsindikiza mama yake.
Gazeti hili lilimtafuta tena Willy na kumweleza kuhusu majibu ya Mzee wa Upako, lakini kijana huyo wa marehemu alisema hataweza kumpeleka mama yake kwa mchungaji huyo kwa sababu bado anapokea wageni wanaokuja kuhani msiba.
“Itakuwa jambo la ajabu kwa mfiwa kuanza kuzunguka huku na kule kufuatilia rambirambi, hiyo siyo kawaida kwa mjane kukusanya rambirambi kwani kanisa liliweka utaratibu,” alisema Willy.
Katika kuaga mwili wa marehemu, Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God Mikocheni B, Dk.Getrude Rwakatare alitangaza rambirambi zake kuwa angetoa shilingi milioni moja, akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Mchungaji Josephat Gwajima aliyeahidi kutoa shilingi milioni 10. Wote wametimiza ahadi zao.
Baadaye alikabidhiwa kipasa sauti Mzee wa Upako ambaye alitangaza kwamba hawezi kuzidiwa na Mchungaji Gwajima, hivyo aliahidi kutoa shilingi milioni 15.

Hata hivyo, baadhi ya wachungaji na maaskofu waliamua kufanya siri ahadi zao.


Source:Global Publishers. 

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza kuanza kutumia huduma ya M-pesa katika kukusanyia marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika hatua ikiwa ni katika mikakati ya bodi ya kuimarisha makusanyo ya urejeshaji wa mikopo hiyo.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Bw. Asangye Bangu amewaambia waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es salaam kwamba bodi inaendelea kujipanga kuhakikisha inaboresha njia za urejeshaji mikopo ili kuwpatia walengwa urahisi.

Amesema mojawapo ya kazi za Bodi ni kusimamia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya elimu ya juu pamoja na urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa na Serikali kwa waliokuwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa kwa nia ya kuufanya mfuko wa Elimu ya Juu kuwa endelevu.

"Tunayofuraha kubwa sana leo kutangaza kwamba sasa wanufaika wa mikopo ya Bodi wanauwezo wa kutumia mfumo wa M-pesa kufanya marejesho ya mikopo yao moja kwa moja kwa Bodi."Alisema Bangu

Bingu amesema bodi inaimani kuwa M-pesa itawapatia urahisi wanufaika kuweza kutimiza wajibu wao kisheria wa kurudisha mikopo waliopatiwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.

Amesema wanufaika wa mikopo wanapaswa kuanza kurejesha mikopo yao mara baada ya miezi 12 kuanzia wanapohitimu masomo ya elimu ya juu au wanapositisha masomo kwa sababu yoyote ile, akiwa ameajiriwa ama hajaajiriwa.

Bingu amesema wanufaika walioajiriwa wanalipa mikopo yao kupitia kwa waajiri wao ambapo hukatwa marejesho ya mikopo kwenye mishahara yao ya kila mwezi na mwajiri huwasilisha makato hayo kwenye Bodi kupitia kwenye akaunti zake huku wale ambao sio waajiriwa hupeleka huwasilisha marejesho ya mikopo katika benki za bodi.

"Wanufaika wanaorejesha mikopo yao kwa pesa taslim wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali wakati wa urejeshwaji wa mikopo yao kupitia kwenye akaunti za Benki ikiwa ni na benki hizo kutokuwa na matawi ya kutosha yaliyokaribu na warejeshaji wa mikopo pamoja na kutumia muda mwingi kwenye foleni."Alisema Bingu "M-pesa itapunguza changamoto hizo na hatimae kuwajengea mazingira mazuri ya urejeshwaji wa mikopo, Bodi inatangaza rasmi kuanza kutumika kwa utaratibu huu mpya wa urejeshaji kwa M-pesa kuanzia sasa."

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim amesema kuzimduliwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa jinsi ambayo huduma ya M-pesa inavyorahisha miamala nchini kuzidi kuwa rahisi.

"M-pesa imekuwa suluhisho la changamoto nyingi zinazohusiana na malipo ama miamala mengine ya kijamii na kibiashara."Alisema Mwalim na kuongeza. "Ni wazi sasa hakuna atakaekuwa na usumbufu katika kulipia mkopo wake kwenye Bodi ni kiasi tu cha kupiga *150*00# na hapo anauwezo wa kufanya mrejesho wake wakati wowote mahali popote."

"Tunaishukuru Bodi kwa kuendelea kuiamini huduma yetu ya M-pesa walianza kwa kuitumia katika ukusanyaji wa ada za uombaji wa mikopo na sasa wanakwenda mbali zaidi kwa kuichagua kuitumia katika makusnayo ya marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika."Aliongeza

Mwalim amesema kwa njia hiyo ni wazi sasa Bodi itashuhudia mabadiliko makubwa kwenye makusanyo ya marejesho kwa kuwa huduma hiyo imeenea nchi nzima na hasa kwa kuwa inauwezo pia wa kumuunganisha mteja na benki yake.

"Kwa mtandao mpana wa huduma hii mawakala na na mtengamano wake na mabenki na jinsi inavyotumika ni wazi mtarajie ufanisi kwa kuwa sasa mmewawezesah wanufaika wa mikopo kuwa na uwezo wa kufanya marejesho kwa njia rahisi zaidi Wakati wowote mahali popote kwa usalama na uhakika zaidi."AAliongeza


Ili mnufaika aweze kulipia kupitia M-pesa anapaswa kwanza kuhakikisha kuwa ana taairfa ya Mkpo(loan Statement),Kiwango cha Marejesho na Nambari ya Kumbukumbu amabvyo vinapatikana ofisi za Bodi hiyo ya mikopo. Taarifa hizo zitatumika Wakati w akulipia baada ya mteja kupiga *150*00# kutoka kwenye simu yake ya Vodacom na kuchagua nambari nne ambayo ni ya malipo na kuendelea na maelekezo kadri yanatakavyokuwa akiyapata kutoka kwenye simu yake ya kiganjani.
Habari tulizozipata zinasema kuwa gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge kwa 2015.


Muigizaji huyu mkongwe mzee Majuto ametangaza  kugombea ubunge jimbo la Tanga mjini.

Majuto  mwenye umri  zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds, na akadai atagombea kupitia CCM.

Bado tunamtafuta mzee majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni kwa kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini.


Je, kama ni kweli, unahisi ataweza? 

Vijana 11 wamekamatwa Mkoani Mtwara wakifanya mazoezi katika msitu wa Makolionga na CD zenye mafunzo ya kigaidi za Al Qaeda na Al Shabab pamoja na zana za hatari.


Polisi mkoani Mtwara imewakamata vijana kumi na moja wakiwa wanafanya mafunzo ya kijeshi kwa kutumia CD za Al Shabaab na Al Qaeda  katika mlima wa Makolionga...CD hizo zinaonyesha mbinu mbali mbali za kijeshi na mauaji .
 Baada ya bosi wa washika mitutu wa jiji la London Arsene Wenger kumuonya kiungo wake Jack Wilshere ambaye alikataa katakata juu ya mwenendo wake wa hovyo wa kuvuta sigara mbele ya hadhira, hatimaye kiungo huyo amekubali kosa na kuahidi kuwa haitatokea tena.
Wilshere amesema kuwa alifanya kosa baada ya kupigwa picha akivuta sigara nje ya ukumbi mmoja wa starehe huko London mida ya usiku.

Bosi wa Wenger aliweka hilo wazi Ijumaa iliyopita ambapo alikaririwa akisema hakubaliani hata kidogo na tabia hiyo na licha ya awali kiungo huyo wa kimataifa wa England kukanusha, sasa amekubali kufanya kuhukumiwa kwa kosa hilo.
Akiongea na mtandao wa klabu hiyo Wilshere amenukuliwa akisema 
"I made a mistake,"

"Players make mistakes. I'm not a smoker.

"Nimeongea na bosi na kunitaka kueleza kilichotokea na nimemueleza na hatimaye kutatua hilo na kunirejesha kikosini na nina matumaini na kumjibu kwa kufunga goli dhidi ya West Brom.

"Haitatokea tena, mimi si mvuta sigara hivyo nadhani hiyo itakuwa ni mara ya mwisho."

 Hizi picha tatu zipo kwenye baadhi ya miezi kwenye calendar hio.



STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma 
Jumamosi iliyopita alikwea pipa kuelekea nchini 
Kenya ambako ana ziara ya siku nne kikazi na 
akiwa humo alipata fursa ya kupewa mguu wa 
bandia bure na wenyeji wake huku pia akiahidiwa kufanyiwa ‘
check-up’ ya mwili mzima.

Leo nimebahatika kukutana na huyu dogo aloimba wimbo ambao mpaka sasa ndo inaongoza kwa kusikilizwa na watu mtandaoni.Imesikilizwa na watu zaidi ya elf 51.Amefunika ngoma zote kali hapa Bongo.Wimbo huo amemchana kaka yake Diamond.Kaelezea maisha yake kabla hajatoka kimuziki.

Swali moja tu la msingi nlotaka kujua kutoka kwake ni Uhusiano wake na Diamond na amekiri kuwa Diamond ni kaka yake wa Damu,Baba moja Mama Tofauti na kadai Diamond kabla hajatoka kimuziki alikuwa anawajali ndugu zake ila kwa sasa hata baba yake mzazi hana muda naye.
Hivyo kadai yote aloimba kwenye huo wimbo ni ukweli mtupu.Ameomba watu kumkumbusha Diamond kukumbuka nyuma,Usuperstar ni maji ya Moto.Tazama PICHA ZAKE KATIKA POZ MBALIMBALI NA Chini kabisa ni wimbo huo ambao ishakuwa gumzo kwa kweli.



KAMA HUNA MBAVU USIDIRIKI KUSIKILIZA WIMBO HUU TAFADHALI.DOGO KAUA AJABU.NI BONGE MOJA LA NGOMA.

Monday, 7 October 2013

A LOOK AT SAMUEL ETO’O



CFC fans who lament the club unfortunately missing out on signing Samuel Eto’o the last time it was seemingly possible in 2006 have their wish now the iconic Cameroonian wears a blue shirt and calls West London home. It would be nigh on ridiculous to argue that if Eto’o had signed for CFC when he was strongly linked seven years ago he wouldn’t have scored a vast amount of goals at important times, contributed heavily and added to the successes of the club during the period. This is now a moot point and consigned to history.

Soccer - UEFA Champions League - Group E - Chelsea v FC Basel - Stamford Bridge


By bringing Eto’o from the Republic of Dagestan back to elite European football CFC have added an undoubted living, playing legend of the game to the Stamford Bridge roster. The move will certainly be proven to have a detrimental effect on any team and defender that calls CFC an opponent over the forthcoming season and ideally beyond. At the age of 32 the typical questions will be asked of Eto’o as they have been of Frank Lampard, Didier Drogba et al during their post-30 years at CFC. Like Drogba and Lampard have done consistently I am sure Eto’o will silence any critics with performance over the coming months.
Without generalising and backing up theory with example one reason to disbelief any age related comments regarding Eto’o is the physicality and stamina that serves players whom herald from the continent of Africa well in the twilight of their careers. Especially in the Premier League. Without constantly referring back to Drogba and his phenomenal exploits for the club in the victorious assault on the Champions League in 2012 throughout which Drogba terrorised the best defences in Europe at age thirty four there are numerous other examples of African players who seem to enjoy their career peak years at a later stage than their European counterparts.
Jay Jay Okocha was a revelation at the Reebok Stadium until he was well into his thirties when he arrived from Paris Saint-Germain and Nwanko Kanu was successful not only at Arsenal but was hugely popular during his veteran years as part of Portsmouth’s FA Cup winning team in 2008. Tony Yeboah is also more than worthy of mention in this respect. Yeboah spent his final peak years as a Premier League cult hero, rightly so as he was the rare combination of a great goalscorer and the scorer of great goals for Leeds United. Finally and by no means least two legendary figures born in Africa (regardless of eventual French allegiance international football-wise) that have woven their names indelibly into the rich tapestry that is CFC’s modern history are Marcel Desailly and Claude Makalélé. Neither need an introduction. Both arrived at CFC at points of their careers that some might term the veteran stage. Both joined CFC, much like Eto’o, having achieved much domestically and on the continent for their previous major European clubs. Both had a monumental impact and were vital to the successes of CFC in their respective eras. The omens for Eto’o are good.
Romania Soccer Champions League
Eto’o has joined CFC as a player with his name etched in elite football folklore who has been followed by success through his career. He is the only player in history to win the treble, (domestic league, cup and Champions League) leave the treble winners moving leagues and countries at the end of season only to repeat the exact same feat the following year. This is of course in reference to his final year with FC Barcelona and his maiden season with José Mourinho’s Internazionale during the period 2008-10. All of this with the backdrop of Eto’o's transfer which saw Barcelona lose their Champions League final goalscorer and €46m to secure the arrival of Zlatan Ibrahimovic in Massimo Moratti’s self-proclaimed best piece of business as Inter premier. It is not a surprise that upon joining forces in Milan Eto’o realised he and Mourinho are kindred spirits – born winners. The player’s introduction into the CFC side should serve to inject a hunger adding to that already in place. The added competition for Fernando Torres and Demba Ba should spur both on to higher levels of performance. This was evident in Torres’ Capital One Cup display at Swindon.
The CV of Samuel Eto’o is too extensive to detail fully. Needless to say he is the most decorated African football player in history. Aside from his trophy cabinet and records held at club level Eto’o has won African footballer of the year a record four times and has achieved much for his native Cameroon at international level. Eto’o is the leading goalscorer in the history of the African Cup of Nations, his goal tally standing at 18 having won the tournament twice. His heroic image in his homeland is owed in part to his status as Cameroon’s most capped player and highest goal scorer with 112 appearances and 55 goals. Eto’o has used his remarkable career and subsequent high profile, especially in Africa, to give back to those struggling on the continent by establishing the Samuel Eto’o Private Foundation. The non-profit organisation was founded in 2006 and operates predominantly in West Africa having its head office in Douala, Cameroon while also having two offices in Spain where Eto’o holds a passport thanks to his many years working in the country.
Broadly speaking the aim of the Samuel Eto’o Private Foundation is the protection of children and young people, provision of emergency aid and encouraging education and health throughout Africa. The projects in which the foundation engages are relied upon and offer remedies to the huge issues faced in region. This is very much a noble cause. Of course the contribution of the foundation is not likely to be the first point made by journalists and the like when discussing Eto’o's fictional selfishness and divisive tendencies in a football dressing room.
Having accomplished so much on and off the field since beginning his career as a professional footballer all that remains for Eto’o is to win his fourth Champions League with CFC and further elevate himself as an immortal legend of game and beyond.
Thanks for reading and keep the blue flag flying high. Written by Dean Evans, you can fol

SHILOLE ATOA YA MOYONI "KUWAPANDISHA JUKWAANI WANAUME NA KUNISHIKA KINAWAFURAHISHA WENGI"



Baada ya watu kuongea sana kuhusu jinsi Shilole anavyo fanya show zake na staili ya kuwapandisha wanaume jukwaani na kucheza nao kwa staili ya nisheke popote.


Amejitokeza na kuongea na chombo kimoja cha habari na kusema yeye hajivunjii heshima kama watu wanavyosema bali anakizi mahitaji ya mashabiki wake..."watu wanapenda sana jinsi navyofanya ...ni njia moja wapo ya kuchangamsha show jukwaani kwahiyo sioni tatizo hapo ...wanaosema najivunjia heshima niwashamba..mimi ni msanii lazima nitafute njia ya kuwapa burudani mashabiki wangu...."

HATUA ya Serikali ya Tanzania kuyafungia magazeti mawili ya kila siku, Mtanzania (kwa siku 90) na Mwananchi (siku 14), imesababisha mjadala wa hali ya juu katika maeneo mbalimbali barani Afrika.


Gazeti la Mail&Guardian la Afrika Kusini, liliandika kuwa hatua hiyo ni kusambaratisha uhuru wa vyombo vya habari na kuwanyima wananchi haki ya kupata habari. 

Gazeti hilo liliendelea kudai kuwa hatua ya kufungia vyombo vya habari ni kuvunja maana ya upashanaji habari, ambayo inatakiwa kuwafikia wananchi. 

Chombo hicho cha habari kimeifananisha adhabu hiyo ya kuyafungia magazeti hayo mawili kama ile iliyochukuliwa na Serikali ya Uganda, mwanzoni mwa mwaka huu ya kulifungia gazeti jingine la NMG, la Daily Monitor, kwa madai lilichapisha habari ya uchochezi.

Tangazo la Serikali ya Tanzania kupitia Gazeti la Serikali namba 333 Septemba 27 mwaka huu lilitangaza magazeti ya Mwananchi na Mtanzania yamefungiwa.

Katika hatua nyingine, gazeti la Mail&Guardian lilimkariri Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akisema kuwa “Kufungia magazeti hakutazuia haki ya wananchi kutoa maoni yao na kupambana mpaka kupatikana utawala bora. 

“Kwanza kufungiwa kwa magazeti hayo kutawaimarisha waandishi kwa kiwango cha juu. Unalifungia gazeti kwa kutoa taarifa za mishahara? Tatizo liko wapi, je, watu hawatakiwi kujua mishahara ya watumishi wa umma?”

Ikitumia Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, iliyafungia magazeti hayo kwa madai ya kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani. Serikali ilitangaza kulifungia Mwananchi kwa siku 14 na Mtanzania siku 90, kuaNzia Septemba 27, mwaka huu. 


Uamuzi huo ulichukuliwa na serikali kwa madai kwamba, magazeti hayo yaliandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola. Uamuzi huo, ambao ulikuwa ghafla, ulipokewa kwa mshituko mkubwa na wadau mbalimbali, huku wengi wakihoji mwelekeo wa demokrasia nchini. Wadau hao wa kada mbalimbali, wakiwamo wanasheria, wanataaluma, wanahabari, wanaharakati, wanasiasa na watetezi wa haki za binadamu, wote wamekuwa na kauli moja ya kufanana.



SOURCE:http://www.udakuspecially.com/2013/10/afrika-kusini-yaguswa-kufungiwa-kwa.html































HALI ya amani katika mji wa Mombasa imezidi kuwa tete kutokana na makundi ya vijana wenye hasira kali kuendeleza machafuko katika sehemu mbalimbali vya mji huo.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BBC, jumla ya watu wanne wamepoteza maisha katika machafuko hayo, baada ya makundi ya vijana hao kupambana na askari wa kutuliza ghasia.


Habari kutoka nchini humo zinaeleza kuwa machafuko hayo yametokea siku moja baada ya kifo cha Sheikh Ibrahim Omar ‘Rogo’, aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Katika shambulizi hilo, pia washirika watatu wa Sheikh Rogo nao wamepoteza maisha papo hapo, huku Salim Adbi akinusurika katika shambulizi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zaidi kutoka mjini Mombasa, vijana wenye hasira kali wameteketeza kanisa moja katika ghasia za juzi. 

Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa mhubiri katika msikiti ambao ulikuwa unatumiwa kwa mahubiri na marehemu Sheikh Aboud Rogo, ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mwaka jana.

Sheikh Aboud Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.

Kabla ya kifo chake, marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Tukio la kifo cha Sheikh Ibrahim Omar ‘Rogo’ limetokea ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya shambulizi la kigaidi la Westgate Mall, ambapo jumla ya watu 67 walipoteza maisha.


Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.

Imeandikwa na Mtanzania

SULUHU ya bila kufungana kati ya Coastal Union na Azam FC katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga imezidi kuwaongezea idadi ya suluhu Wagosi wa kaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.


Mchezo huo uliokuwa na presha kubwa kwa mashabiki na wachezaji ulimuweka katika wakati mgumu mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani, kutokana na kushutumiwa kuwapendelea Azam FC.

Kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa nguvu zikihakikisha zinapata mabao ya mapema na kujihakikishia ushindi lakini hakuna hata timu moja iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam FC kushambulia kwa kasi huku wakimiliki mpira hali iliyowachanganya wachezaji wa Coastal Union wakaanza kupoteana na kucheza bila kufuata mfumo. Hali hiyo ilizidi kuwachanganya Wagosi wa Kaya hasa baada ya mwamuzi kuanza kutoa maamuzi ya utata, kwani katika dakika ya sabini alitoa kona kwa Azam wakati ilikuwa ni goal kick.

Mashabiki wakaanza kuhamaki na kutaka kuvuruga mchezo baada ya mwamuzi kuzidisha kutoa maamuzi ya utata kama faulo zisizoeleweka na kona za utata. Hali hiyo ilimtisha mwamuzi na kusimamisha mchezo mara kwa mara ili kuwataka wasimamizi wa mchezo huo kuwatuliza mashabiki.

Tukio lililotokea kipindi cha kwanza ambapo mwamuzi wa pembeni alipigwa na kitu kisichojulikana kutoka jukwaa la 'Rasha' lilitaka kujirudia kipindi cha pili baada ya chupa na mawe kutupwa uwanjani baada ya mwamuzi kutoa faulo nje kidogo ya 18 upande wa Coastal Union.

Dakika ya 65 mwalimu Hemed Moroco alifanya mabadiliko na kumtoa Pius Kisambale akaingia Suleiman Kassim 'Selembe'. Mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa Wagosi hasa kutokana na aina ya uchezaji wa Selembe kutumia mipira ya kasi.

Azam FC walianza kuelemewa kutokana na Mganda, Yayo Kato kutumia vema mwili wake mfupi na wenye nguvu kuwashambulia mabeki wa Azam, hali hiyo iliwafanya Azam kubadilika na kucheza mpira wa hovyo uliowapa nafasi Coastal Union kupiga mipira mirefu ambapo ilipofika dakika ya 75 kipindi cha pili katika jukwaa la African Sports, Wagosi walikosa bao la wazi baada ya Selembe kupiga krosi iliyopenya ngome ya Azam akiwemo mlinda mlango Mwadini Ally na kugonga mwamba.

Kutokana na piga nikupige ya lala salama kufika dakika ya 74 mwamuzi alimnyooshea mlinzi wa kulia wa Coastal Union, kinda Hamadi Juma 'Basmat', kadi nyekundu baada ya kubadilishiana maneno na mchezaji wa Azam, Kipre Tchetche.

Tukio hilo lilianzia kwa Kipre kumpiga Hamadi kiwiko cha shingo hali iliyomfanya kinda huyo kumfuata kwa jazaba huku akimuuliza kwanini amemfanyia hivyo. Mwamuzi baada ya kuona Hamadi amemuelekezea kichwa Kipre akadhani kinda huyo anapigana ndipo akatoa kadi ya moja kwa moja.

Baada ya kadi hiyo hali ya uwanja ilichafuka ambapo mashabiki walikuwa wakipiga kelele huku wachezaji wakitaka kupigana, ndipo mchezaji mwingine wa Coastal Union beki wa kushoto Othman Tamim akapewa kadi ya njano papo hapo.

Baadaye mchezo ulirudi katika hali yake lakini ngome ya Coastal Union ilikuwa imepwaya hali iliyomfanya Juma Said 'Nyoso' kuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha ngome yao inakuwa imara.

Ilipofika dakika ya 84 mwlimu Moroco alifanya mabadiliko kwa kumtoa Uhuru Suleiman na kumuingiza Yusuf Chuma. Ambapo kinda huyo alionyesha uwezo mkubwa na kurudisha uhai wa safu ya ulinzi.

Mpaka mwamuzi wa leo anapuliza kipyenga cha mwisho matokeo yaliendelea kusomeka hivyo hivyohivyo 0-0, na kuendelea kuibakisha Coastal Union katika nafasi ya nne ikiwa na point 11 nyuma ya Azam iliyo nafasi ya tatu yenye point 11 lakini ikiwa na mabao mengi ya kufunga.

Baada ya mechi ya leo Coastal Union itashuka dimbani wiki ijayo katika uwanja wa Chamazi dhidi ya Ashanti United wanaoshika mkia katika ligi.