Ziara ya Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama, imetosha kudhihirisha kwamba hakuna kiongozi mwenye mvuto na anayelindwa duniani kote kama yeye.

Inaweza kuonekana pengine ulinzi wake umeimarishwa Afrika tu lakini ripoti zinaonesha kwamba kiongozi huyo hulindwa kwa nguvu kubwa kokote kule aendako.
Ulinzi wa Obama akiwa nchi za Afrika wikiendi iliyopita, unalingana na ule ambao uliwekwa Mei, 2011, alipokwenda Uingereza.

Maandalizi pekee ya ziara yake ni kipimo tosha kwamba Obama hana mfano wake duniani kote kwa sasa.
Ukichanganya na ulinzi anaopewa, mvuto wake kijamii ni mkubwa ndiyo maana ziara yake imekuwa ya kipekee duniani kuliko yoyote ile iliyowahi kufanywa na kiongozi mwingine ulimwenguni kote.
DAR YATIKISIKA
Kuelekea ujio wa Obama, Jiji la Dar es Salaam limetikisika kwa kiasi kikubwa na kusababisha ofisi zifungwe na wafanyakazi wengine kujipa likizo bila kufuata utaratibu.
Ugumu wa watu kufika katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakati wote wa maandalizi ya ujio wa Obama, ndiyo kichocheo cha wengine kujipa likizo mpaka hapo kiongozi huyo atakapoondoka kurudi nchini kwake.
Baadhi ya ofisi zinazotegemea mauzo ya siku, zimefungwa kwa sababu mzunguko wa kibiashara haukuwa mzuri kuanzia wiki mbili kabla ya ujio wa Obama.
Magari ya abiria, yaani daladala na teksi nyingi zilisitisha kutoa huduma kwa muda kwa sababu ya kukwepa hasara, kutokana na ukweli kwamba abiria walipungua kwa kiasi kikubwa.

WAMACHINGA WALIA
Kishindo cha Obama, kimewagusa mpaka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga ambao wamelia kitendo cha kuondolewa katikati ya jiji.
Mfanyabiashara Maneno Kisala alisema: “Hivi sasa maisha yangu yamekuwa magumu. Kipato ambacho nilikuwa nakipata hapa na kula na familia yangu sasa sikipati.”
Mwingine, Henry Kilado alilalamika: “Tunajua Obama anakuja kwa faida kubwa ya nchi yetu lakini dah, maisha yamekuwa magumu sana. Inabidi serikali ifikirie namna ya kutuacha tufanye biashara, usalama ungedumishwa kwa njia nyingine tu.
“Sisi siyo magaidi, nchi yetu ni salama. Vyombo vya usalama vingetusimamia lakini vingetuacha tufanye kazi zetu vizuri.”
AJA NA NDEGE 20
Obama, anatembea kwa kutumia ndege yake ya Air Force One ambayo ni maalum kwa ajili ya Rais wa Marekani lakini pamoja naye, zipo ndege nyingine 20.
Ndege hizo 20 ndizo ambazo zimekuja nchini na makachero watakaomlinda kiongozi huyo katika kipindi chote atakachokuwepo Tanzania.
Taarifa zinasema katika ndege hizo 20, ya mwisho iliwasili Jumapili iliyopita mchana na timu ya walinzi iliratibu kila kitu kabla ya Obama kuwasili.

MAGARI 150
Meli mbili na manowari kubwa ya kivita, vimewasili nchini kwa ajili ya kudumisha ulinzi wa Obama kipindi chote akiwa nchini.
Magari 150, yamewasili nchini, hayo yalibebwa na ndege kubwa tatu, kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba magari 50, siku kadhaa kabla hajawasili nchini.
Uwepo wa magari hayo una maana kuwa msafara wa Obama hautaingiliwa na mengine, vilevile lengo kuu ni kwamba lazima sura ya kiongozi huyo anapotembea ndani ya Marekani, ifanane na akiwa nje.
MAREKANI NI TISHIO KWA TEKNOLOJIA
Zipo helikopta kadhaa ambazo ziliwasili nchini vipandevipande na kuunganishwa hapahapa.
Helikopta hizo, kazi yake ni kufanya doria kipindi chote cha kabla ya Obama hajawasili nchini na muda wote akiwa ndani ya nchi.
Wikiendi iliyopita, makachero wa Marekani walikuwa na kazi nzito ya matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria.
Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipandevipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili.
Habari zinasema kuwa helikopta hizo sita, ziliunganishwa katika sehemu ya karakana ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).


 Huyu ndiye malaika wa Mungu aliyetelekezwa maeneo ya bamaga nje ya chuo cha ustawi wa jamii karibu na TBC hapa akiwa amebebwa na mmoja wa mfanyakazi wa ITV baada ya wasamaria wema kumleta ITV,Anayeonekana kwa nyuma ni mmoja wa vijana waliomuokota mtoto huyo.
 Hembu angalia jinsi katoto kalivyo kazuri kenyewe kanahisi kako na mama yake 
kumbe msamaria mwema.
 
 
 
 
source:Mchome blog 






MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemtia hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).

Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.

Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shitaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.

Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana na mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti ana umri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.

Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimharibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani , hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha.

Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kuhusu kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madai kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.

Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.

Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.

Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi
   MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela

  Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
  Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
 Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika


Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini  baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30

  Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha

Mbeya yetu 
Huyu  ni Fezza Kessi akifanya upuuzi wake mjengoni.



DSC 0157 db3db
DSC 0163 0cc83
DSC 0162 fd06c
DSC 0158 c75a3
DSC 0159 22c0d
DSC 0160 bc092
DSC 0161 a3658
DSC 0164 0d0d6

Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.


Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo....

Tunapenda  kuungana na  Rais Jakaya  Kikwete na  watanzania  wote  wapenda amani katika  kumshukuru Rais wa Marekani Barack Obama kwa  kuichagua  Tanzania...

Pia tunawapongeza  watanzania  wote kwa kuonyesha umoja  wetu na hata  kuzika itikadi zetu za kisiasa   na   hata  kupelekea  TV zaidi ya 1000 duniani na radio zaidi ya  3000 duniani  kuitazama  Tanzania.

JACKSON Ngechu Makini ‘CMB Prezzo’ alizaliwa siku ya Jumatano ya Januari 09, mwaka 1980. Ni rapa wa Kenya ambaye alikuwa mmoja wa mastaa waliowakilisha nchi zao katika Shindano ya Big Brother Africa ‘StarGame’, 2012.


Alizaliwa katika Jiji la Nairobi miaka 33 iliyopita, alikulia maisha ya kitaani eneo la Eastleigh.


Prezzo ni mwanamuziki mkubwa ambaye alianza ‘kuhaso’ katika muziki miaka mingi,lakini alikuja kuwika kwenye miaka ya mwanzoni mwa karne ya 21.


Pamoja na kukumbana na vipingamizi vingi, nyota ilikuja kung’aa baada ya nyimbo zake kukubalika kwa maelfu ya mashabiki wake waliokuwa wakizisikiliza, kuziomba kwenye stesheni mbalimbali za redio na runinga huku wakihudhuria katika matamasha yake ya wazi na klabu.


Albam yake ya kwanza ni Naleta Action aliyoiachia mwaka 2004 ikiwa na ngoma zilizoshika kama Naleta Action, Lets Get Down, Mahangaiko, Leo ni Leo, Mimi na Wewe, Mafans na nyingine kibao.


Katika albam hiyo, jamaa alimshirikisha mama yake ambaye aliimba mistari kadhaa katika moja ya nyimbo zake.


Albam hiyo iliuza nakala nyingi na kumfanya Prezzo kuamini kuwa alishakubali Afrika Mashariki kutokana na aina ya ngoma zake zenye hisia.


Prezzo anajulikana kutokana na aina ya maisha ya gharama anayopendelea kama kuvaa mikufu ya bei ghali, nguo, magari na vitu vingine vya kitajiri.


Baadaye mtu mzima Prezzo alishirikishwa kwenye ngoma ya Tazama Mbele ya aliyewahi kuwa mpenzi wake wa kipindi hicho iliyotengenezwa na Ennovator wa Samawati Productions huku video yake ikisimamiwa na Ted Josiah.


 Ngoma hiyo ilifanya vizuri kwa kushika namba moja kwa wiki nane katika stesheni mbalimbali za redio na runinga Afrika Mashariki.

Mwaka 2006, Prezzo aliachia singo mpya ya P.R.E.Z.Z.O ambapo video yake ilisimamiwa na Ted Josiah wa Blu Zebra. Video ilikuwa kali lakini ilikutana na maneno mengi ikidaiwa ilitengenezwa kwa gharama kubwa sana ya Sh. 500,000 za Kenya. 


Hakukuwa na video iliyokuwa imetumia kiasi hicho cha fedha kwa wakati huo.

Ulipita ukimya kidogo, akiendelea kugonga shoo za ndani na nje ya Afrika Mashariki, Nigeria na Ulaya. Baadaye aliendelea na mtindo wa kuachia singo mojamoja kama Liqher, My City My Town, Unataka Nini, 4sho 4shizzy aliyomshirikisha Ulopa, Nipe Nikupe aliofanya na AY na Celebration of Life aliyoachia hivi karibuni akimshirikisha Chess.

BIG BROTHER AFRICA ‘STARGAME’ 2012
Prezzo aliingia kwenye kinyang’anyiro cha BBA ‘StarGame’ 2012 baada ya kuona ni kitu kitakachompa changamoto nyingi kwenye maisha.